Thursday, July 19, 2018

Waandishi wa Habari za Mahakama Wafanya Mafunzo kwa Vitendo Mkoani Morogoro


1
Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro Mhe. Elizabeth Nyembele akizungumza na waandishi wa habari leo wakati walipotembelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro kwenye moja ya ziara za kimafunzo wakiwa katika semina ya Waandishi wa habari za mahakama mkoani Morogoro
2
Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro Mhe. Elizabeth Nyembele akizungumza na wananchi waliokuwa wakisubiri kuanza kwa mashauri yao  kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro katika  ziara ya kimafunzo kwa waandishi wa habari wakiwa kwenye semina ya uandishi  wa habari za mahakama mkoani Morogoro
(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-MOROGORO)
3
Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro Mhe. Elizabeth Nyembele akizungumza na waandishi wa habari   katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro kwenye ziara ya kimafunzo kwa waandishi wa habari wakiwa kwenye semina ya uandishi  wa habari za mahakama mkoani Morogoro
4
Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro Mhe. Elizabeth Nyembele akionyesha waandishi wa habari nembo ya  iliyopo  kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro kwenye  ziara ya kimafunzo kwa waandishi wa habari wakiwa katika semina ya uandishi  wa habari za mahakama mkoani Morogoro
5
Baadhi ya waandishi wa habari wakisikiliza maelezo ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro Mhe. Elizabeth Nyembele hayupo kwenye picha.
6
Mtendaji Mkoa wa Mahakama Nestory Mjunangoma amesema akitoa maelezo kwa waandishi wa habari wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi wa mambo kadhaa kwa wanahabari.
7
Baadhi ya wanahabari wakiendelea na ziara yao.
8
Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro Mhe. Elizabeth Nyembele akimsikiliza mmoja wa waandishiwa habari wakati wa ziara hiyo ya kimafunzo.
……………………………………………………………………………………….
Na Lilian Lundo na Beatrice Lyimo-MAELEZO, Morogoro
Waandishi wa habari za Mahakama wamefanya mafunzo kwa vitendo katika Mahakama za Mkoa wa Morogoro ili kuona namna Mahakama hizo zinavyotekeleza majukumu yake ya kila
siku.
Lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha wadau wa mahakama wakiwemo waandishi wa habari wanakuwa na uwezo wa kuwahudumia wananchi kwa weledi.
Akitoa maelekezo namna mahakama zinavyofanya kazi, Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro Mhe. Elizabeth Nyembele amesema kuwa , katika mahakama zipo kesi zinazosikilizwa katika Mahakama za wazi na nyingine husikilizwa Mahakama za ndani( Chamber).
” Kesi zote zinazohusu unyanyasaji wa kijinsia mfano ubakaji, kesi za mambo ya ndoa au kesi yoyote ambayo itamhusisha mtoto kesi zao husikilizwa katika mahakama za ndani ( Chamber)” ameongeza Mhe. Hakimu Nyembele.
Aidha, Mhe. Hakimu Nyembele amesema kuwa kwa mkoa wa Morogoro wamekuwa wakipokea kesi nyingi zinazohusiana na masuala ya unyang’anyi, madawa ya kulevya na ujangili unaosababishwa na mkoa huo kuzungukwa na mapori.
Akizungumza kuhusu suala la rushwa kwa makarani wa mahakama, Mhe. Nyembele ametoa rai kwa watumishi wote wa mahakama kuepuka kupokea rushwa na kuwa waaminifu katika utendaji wao.
Vilevile amesema kuwa katika kudhibiti suala la rushwa katika mahakama nchini, mahakama imetoa elimu kwa umma pamoja na matangazo ya huduma mbalimbali za kimahakama zinazotolewa bure mfano nakala za hukumu.
Kwa upande wake, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Morogoro Mjini Mhe. Agnes Ringo amesema kuwa kwa sasa kuna utaratibu mpya wa namna kesi za watoto zinavyoendeshwa bila kutoa utambulisho rasmi wa mtoto husika.
Nae Mtendaji Mkoa wa Mahakama Nestory Mjunangoma amesema kuwa katika mkakati wa kuboresha huduma za mahakama, Mahakama mkoa wa Morogoro inatarajia kuanza ujenzi wa ghorofa nne katika mwaka huu wa fedha zitakazokuwa na huduma zote za kimahakama kuanzia Mahakama ya Mwazo hadi Mahakama Kuu.
Aidha, Mjunangoma ameongeza kuwa ujenzi huo unatarajiwa kukamilika mwaka 2020.
Mafunzo hayo ni moja ya mradi wa maboresho ya huduma za mahakama inayotekeleza programu mbalimbali chini ya mpango mkakati wa mahakama wa miaka mitano 2015/2016-2019/202 iliyoandaliwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia.

No comments :

Post a Comment