Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Mkuu wa
Utafiti na Mkurugenzi wa Mpango wa kusaidia Mabadiliko ya Kiuchumi
kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Kimataifa (ODI) kutoka nchini Uingereza
Dkt. Dirk Willem te Verde mara baada ya kumaliza mazungumzo ,Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya
pamoja na Mkuu wa Utafiti na Mkurugenzi wa Mpango wa kusaidia Mabadiliko
ya Kiuchumi kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Kimataifa (ODI) kutoka
nchini Uingereza Dkt. Dirk Willem te Verde (kulia), Waziri wa Fedha na
Mipango Dkt. Philip Mpango (kushoto) pamoja na wajumbe wengine
walishiriki mkutano huo ,Ikulu jijini Dar es Salaam.(
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye mkutano
na Mkuu wa Utafiti na Mkurugenzi wa Mpango wa kusaidia Mabadiliko ya
Kiuchumi kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Kimataifa (ODI) kutoka nchini
Uingereza Dkt. Dirk Willem te Verde na Ujumbe wake ,Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
………………..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na Mkuu wa
Utafiti na Mkurugenzi wa Mpango wa kusaidia Mabadiliko ya
Kiuchumi
kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Kimataifa (ODI) kutoka nchini Uingereza
Dkt. Dirk Willem te Verde na Ujumbe wake ,Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais amesema Ujumbe huo unataka kutoa ushirikiano katika mpango wetu wa uchumi wa viwanda Tanzania.
Katika mkutano huo ambao pia
ulihudhuriwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango pamoja na
Viongozi na Wataalam wa masuala ya Viwanda na Uchumi nchini.
Nae, Waziri wa Fedha na
Mipango Dkt. Philip Mpango amesema kuwa Taasisi hiyo imekuja kufanya
mazungumzo na Serikali ili kuharakisha utekelezaji wa Mpango wa
Kiuchumi.
Kwa upande wake Mkuu wa
Utafiti kutoka Taasisi hiyo Dkt. Dirk Willem te Verde ameahidi kutoa
ushirikiano wa kutosha kwa Serikali ya Tanzania katika kufanikisha
mpango wa kuwa na Tanzania ya Viwanda.
No comments :
Post a Comment