Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla
akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima mtego wa misumari
uliotegwa na watu wasiojulikana kwa lengo la kuzuia msafara wake wakati
wa ziara yake ya kutatua mgogoro wa mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti na vijiji jirani katika wilaya ya Tarime mkoani Mara jana.
Tarime – Mara
……………………………………………….
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla
ameliagiza Jeshi la Polisi wilaya ya Tarime mkoani Mara kumkamata na
kumfungulia mashtaka Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi
(UVCCM) wa Wilaya hiyo, Newton Mongi na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya
wilaya hiyo, Richard Tiboche kwa tuhuma za kuikashifu Serikali na
kuchochea mgogoro wa mpaka kati ya hifadhi ya Serengeti na vijiji
jirani.
Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo jana majira
ya saa tatu usiku baada ya kuhitimisha ziara yake wilayani humo
iliyolenga kutafuta suluhu ya mgogoro uliodumu kwa miongo kadhaa kuhusu
mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji jirani ikiwemo kijiji
cha Kegonga.
Akiwa njiani majira ya saa tatu za
usiku kwenye gari la wazi baada ya kukagua eneo hilo la mpaka kwa zaidi
ya masaa sita, Waziri Kigwangalla na msafara wake walikuta lundo la mawe
yakiwa barabarani ndani ya eneo la hifadhi hiyo, hali iliyosababisha
taharuki kubwa na msafara wake kushuka na kuanza kuondoa mawe hayo ili
kupata njia ya kupita.
Wakati zoezi hilo likiwa linaendelea,
Kiongozi huyo wa UVCCM alisikika akiituhumu Serikali kwa kuweka mawe
hayo na kwamba hayakuwekwa na wananchi wa eneo hilo, jambo lililozua
mshangao mkubwa kwa viongozi wa Serikali waliokuwepo katika msafara huo
akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima.
Mkuu huyo wa mkoa alisema tukio hilo sio la
mara ya kwanza na kwamba limewahi kuripotiwa mara nyingi na uongozi wa
hifadhi hiyo kuwa wananchi wa vijiji jirani hujaza mawe barabarani kwa
ajili ya kuzuia magari ya doria ili waweze kulisha mifugo yao ndani ya
hifadhi hiyo. Alisema hata msafara wa tume ya Waziri Mkuu Mstaafu,
Mizengo Pinda iliyoundwa na CCM hivi karibuni kufuatilia mgogoro katika
eneo hilo nao ulizuiliwa kwa mawe barabarani.
Imedaiwa pia kuwa kwa nyakati tofauti
viongozi hao wamekuwa wakiwatolea viongozi wa Serikali maneno ya kejeli
pamoja na kuwakwamisha kutekeleza majukumu yao ya kuwahudumia wananchi
ipasavyo.
Awali, kabla ya tukio hilo la mawe barabarani moja ya
gari lililokuwa likiongoza msafara huo lilipata pancha baada ya
kukanyaga misumari iliyokuwa imetengwa kwenye moja ya barabara
zinazoingia na kutoka ndani ya Hifadhi ya hiyo ya Serengeti.
Waziri Kigwangalla alisikitishwa na kitendo hicho
ambacho alikielezea kuwa sio cha kiuungwana kwa kuwa kinalenga
kudhoofisha juhudi za Serikali kumaliza mgogoro huo kwa faida ya pande
zote.
“Mimi ni Muislam, nimesikia kwa masikio yangu
na wala sijaambiwa na mtu yeyote na siwezi kumsingizia mtu,
nimeshangazwa sana na kiongozi tena mtendaji wa chama tawala anawezaje
kuitukana Serikali, na hapa sisi tumekuja kuwahudumia wananchi” alisema
Dk. Kigwangalla kwa masikitiko makubwa.
Wakati huo huo, Waziri Kigwangalla ametoa
miezi mitatu kwa wananchi wote waliovamia ndani ya Hifadhi ya Serengeti
na eneo la wazi (buffer zone) ambao wanaendesha shughuli zao ikiwemo
kilimo, ufugaji na makazi kuachia maeneo hayo kwa hiari yao wenyewe, na
kwamba muda huo ukipita wataondolewa kwa nguvu na chochote
kitakachokutwa ndani ya eneo hilo kitatekezwa kwa mujibu wa sheria.
Akizungumzia kuhusu suluhu ya mgogoro huo wa
mpaka amesema, Serikali itaunda timu ya wataalam kutoka wizarani kwake,
wizara ya ardhi, uongozi wa mkoa wa Mara na wilaya ya Tarime ambao
watashirikiana na watu wengine huru watakaochaguliwa na wananchi wa
vjiji husika wakiongozwa na mbunge wao, John Heche ambao watakuwa na
uelewa wa kusoma ramani na kutafsiri mipaka ili kushirikiana kuhakiki
mipaka halisi ya eneo hilo na kufikia muafaka.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla
(kulia), Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (kushoto) na viongozi wengine
wa mkoa huo wakiangalia mawe yaliyowekwa njiani kuzuia msafara wake
kutoka ndani hifadhi ya Serengeti na watu wasiojulikana wakati wa ziara
yake ya kutatua mgogoro wa mpaka kati ya hifadhi hiyo na vijiji jirani
jana usiku.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla,
viongozi wa mkoa wa Mara na wananchi wa vijiji vinavyopakana na Hifadhi
ya Taifa ya Serengeti wakikagua eneo la mpaka lenye mgogoro kati ya
vijiji na hifadhi hiyo wakati wa ziara yake ya siku moja katika wilaya
ya Tarime mkoani Mara jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla
akiteta jambo na Mbunge wa Tarime John Heche wakati wa ziara yake ya
kutatua mgogoro wa mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji
jirani katika wilaya ya Tarime mkoani Mara jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla
akioneshwa eneo lenye mgogoro wa mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti na vijiji jirani na Mbunge wa Jimbo la Tarime, John Heche
wakati wa ziara yake ya kutatua mgogoro huo mkoani Mara jana. Katikati
aliyeinama ni Mkuu wa Mkoa huo, Adam Malima.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla,
viongozi wa mkoa wa Mara na wananchi wa vijiji vinavyopakana na Hifadhi
ya Taifa ya Serengeti wakikagua eneo la mpaka lenye mgogoro kati ya
vijiji na hifadhi hiyo wakati wa ziara yake ya siku moja katika wilaya
ya Tarime mkoani Mara jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi
Kigwangalla, viongozi wa mkoa wa Mara na wananchi wa vijiji
vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakikagua eneo la mpaka
lenye mgogoro kati ya vijiji na hifadhi hiyo wakati wa ziara yake ya
siku moja katika wilaya ya Tarime mkoani Mara jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla
akisoma taarifa mbalimbali kuhusu mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti
na vijiji jirani vya wilaya ya Tarime mkoa wa Mara wakati wa ziara
yake ya siku moja katika wilaya ya Tarime mkoani Mara kwa ajili ya
kutatua mgogoro wa mpaka kati ya vijiji na hifadhi hiyo jana. Kulia ni
Mkuu wa Mkoa wa Ma
No comments :
Post a Comment