Tuesday, July 17, 2018

MUHIMBILI YAMUAGA MRATIBU WA MADAKTARI WA CHINA


001
Mratibu aliyemaliza muda wake wa timu ya madaktari wa China wanaotoa huduma za afya nchini, Sao Tao akichangia damu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam. Baada ya Tao kuchangia damu, uongozi wa hospitali hiyo ulimkabidhi cheti cha shukrani kutokana na kuhudumu kwa miaka tisa.
002
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akiwa na mratibu huyo, Sao Tao baada ya kumkabidhi cheti cha shukrani.
003
Prof.Museru akimvisha skafu, Sao Tao baada ya kuchangia damu katika hospitali hiyo.
004
Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Museru akiwa katika picha ya pamoja na Sao Tao. Wengine ni watumishi wa Idara ya Maabara Kuu- Muhimbili.

No comments :

Post a Comment