Diwani
wa Viti Maalumu, Grace Kubilima (CCM), ambaye pia ni mkazi wa Kijiji
cha Ihanga, akimshukuru Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, baada ya
kuzindua umeme jana usiku katika kijiji hicho.
Waziri
wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha
Ihanga Wilayani Chato usiku wa jana baada ya kuzindua umeme
Waziri
wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha
Ihanga Wilayani Chato usiku wa jana baada ya kuzindua umeme
NA MWANDISHI WETU, CHATO
WAZIRI wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, ameendelea na ziara yake
vijijini y kukagua miradi ya umeme REA III inayoendelea huku akilazimika
kuzindua umeme usiku.
Amesema amelazimika kufanya uzinduzi huo usiku ili kutoa maana
halisi ya uwepo wa mwanga wa umeme kwa wananchi ili nao waone hali halisi
kuliko ya jinsi raha ya umeme ilivyo.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ihanga Wilayani Chato,
alisema kuwa Serikali pamoja na watalaamu wa Shirika la Umeme Tanzania
(Tanesco) kwa kushirikiana na REA wamekuwa wakifanyakazi usiku na
mchana ili kuhakikisha kazi ya uunganishaji umeme inafanyika kwa
maslahi ya wananchi na kuvutia wawekezaji hasa wa viwanda.
“Ninawashukuru sana wananchi kwani watu wengi wana shauku ya
umeme na kila unapokwenda ukiwaambia leo ninakuja kuwaunganishia umeme wako
tayar kusubiri mpaka usiku, niwapongeze wananchi kwa kweli walikuwa na shauku
kubwa na leo wamepata furaha.
“Na mimi kama mbunge wao bahati nzuri ni Waziri wa Nishati
ilikuwa ni lazima kuwatembelea hata kama ingekuwa usiku. Lakini pia huu ni
mwanga ili udhibitishe kama ni mwanga ni vizuri ukawasha usiku ikaonekana kuwa
kweli hii ni taa. Nadhani walitaka wajiridhishe na wameshuhudia kwa sababu
tumewasha usiku na kwangu nitatembea usiku na mchana kuwatumikia Watanzania ili
mradi nitahakikisha wanapata maendeleo,” alisea Dk. Kalemani
Akizungumzia suala la nguzo za umeme, Dk. Kalemani, alisema kuwa
kwa sasa nchi ina nguzo nyingi kwani kwa mwezi huingizwa zaidi ya nguzo
118,000 na si 2000 kama ilivyokuwa nyuma.
Alisema kuna kampuni 21 za zinatosambaza nguzo nchini.
“Zamani tulikuwa na wasambazaji nguzo watano lakini kwa sasa
tuna kampni 21 hiyo imetokana na kusitisha uagizaji wa nguzo kutoka nje ya nchi
ambazo zilikuwa na gharama kubwa sana kwa Shirika letu la umeme Tanesco lakini
hata wakandarasi. Sasa hivi nguzo wazalishaji wa nguzo ni wengi kwani hata
gharama zimeshuka na pia suala la transfoma si changamoto.
“Mradi unapoanza wanaleta nguzo kutokana na mahitaji kutokana na
eneo husika leo wameanza na nguzo chache lakini kadri ya wananchi
wanavyojiandisha magari huleta nguzo nyingi zaidi ili kuweza kutoa huduma ya
kuunganisha umeme. Na wiki ijayo wataleta nguzo nyingine 200 ombi langu
wananchi wajiandikisha na kulipia ili nguzo ziendele kuwa nyingi.
“Watanzania wana shauku ya kulipia umeme sasa Serikali imekuja
na mpango wezeshi badala ya wananchi kwenda Tanesco sasa litaanzishwa dawati
dogo katika maeneo ya vijiji ili kuwapunguzia gharama za kutembea umbali mrefu.
“Pia wananchi wanaweza kulipia kidogo kidogo na pindi
wanapofikisha Shilingi 27,000 ataunganishiwa huduma ya umeme,” alisema Dk.
Kalemani
No comments :
Post a Comment