Mbunge wa Jimbo la Arumeru
Mashariki,Joshua Nassar akizungumza jambo na Rais Mstaafu wa Marekani
,Barack Obama walipokutana nchini Afrika Kusini akiwa ni miongoni mwa
Viongozi vijana 200 kutoka mataifa 44 ya Afrika waliochaguliwa
kushiriki Programu ya OBAMA AFRICA LEADERS PROGRAM.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru
Mashariki,Joshua Nassar kwa pamoja na Rais Mstaafu wa Marekani ,Barack
Obama wakiwajibika kwa kufanya kazi za mikono katika kuboresha
miundombinu ya shule ya Far North School iliyopo pembezoni mwa jiji la
Johannesburg nchini Afrika Kusini.
Rais Mstaafu wa Marekani ,Barack Obama
akipeana mikono na washiriki wengine wa Programu ya Viongozi wa Afrika
mara baada ya kumaliza kazi za mikono katika shule hiyo.
Mbali na kushiriki kazi za mikono Rais
Mstaafu wa Marekani,Barack Obama pia alipata nafasi ya kutoa mada katika
kongamano lililowashirika viongozi vijana 200 kutoka mataifa 44 ya
Africa.
Wengine waliowasilisha mada katika
Kongamano hilo ni pamoja na Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa (UN)
Koffi Annan ,Rais wa Kwanza Mwananmke Barani Afrika na Rais Mstaafu wa
Liberia ,Ellen Johnson Sirleaf
Pia Mjane wa Rais Mstaafu wa Afrika
Kusini ,Mama Graca Machel alikuwa ni miongoni mwa viongoz walioshiriki
kutoa mada kwa washiriki wa kongamano hilo.
Muanzilishi na Mmiliki wa Kampuni ya
Celtel na muasisi wa Taasisi ya Mo Ibrahim Foundation inayoshiriki
katika utoaji wa tuzo malumu kwa viongozi mbalimbali wa bara la Africa
waliofanya vizuri,Mo Ibrahim pia alishiriki katika kutoa mada katka
Kongamano hilo.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki
,Joshua Nassar akiwa na vijana wengine wa Kitanzania wakishikilia
Bendera ya Taifa wakati wa Kongamano hilo lililoandaliwa na Taasisi ya
Obama Foundation.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassar akiwa na Waziri wa Viwanda ,Biashara na uwekezaji Botswana Bogolo Kenewendo .
Mbunge wa Jimbo la Arumerua Mashariki
,Joshua Nassar akiwa na Waziri wa Ubunifu na Mafunzo ya Ufundi nchini
Cape Verde ,Pedro Lopez.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki
,Joshua Nassar akiwa na mmoja wa Familia ya Mmiliki wa Klabu ya
Mancheter United ,Malcolm Glazer,walipokutana wakati wa Kongamano
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar amesema
ushiriki wa Viongozi vijana wa Kiafrika Katika Kongamano lililoandaliwa na
Taasisi ya Rais Mstaafu wa Marekani ,Barack Obama ,Obama Foundation ni chachu kwa viongozi walioko
madarakani kuendelea kuwamini kwa kuwapa nafasi za ju za uongozi .
Nassar ametoa kauli hiyo zikiwa zimepita siku chache tangu
ashiriki Kongamano lililoandaliwa na taasisi ya Obama Foundation na
kuwashikisha vijana 200 kutoka mataifa 44 barani Afrika wanaofanya kazi serikalini ,asasi za kiraia na
sekta binafsi ambao walikutana kwa muda wa siku tan katika jiji la Johannesburg
nchini Afrika Kusini.
Amesema katika Kongamano hilo kama vijana wamejifunza mambo
mengi ambayo kwa kiasi kikubwa yatachangia kujitokeza kwa vijana wengi zaidi katika
kuwania nafasi mbalimbali za uongozi watakaosaidia kuleta mabadiloko chanya
katika bara la Africa.
Katika kongamano hilo lililoenda sambamba na sherehe za
kilele cha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa muasisi wa taifa la
Afrika Kusini ,Nelson Mandela,vijana nane kutoka Tanzania walichaguliwa
kuiwakilisha nchi ya Tanzania.
Miongoni mwa Viongozi na watu Mashuhuri walioshiriki katika
utoaji wa mada katika kongamano hilo ni pamoja na Rais Mstaafu wa Marekani
,Barack Obama,Rais Mstaafu wa Liberia,Ellen Johnson Sirleaf, Katibu Mkuu Mstaafu wa UN,Koffi Annan na Mmiliki
wa Kampuni ya Celtel na Muasisi wa taasisi ya Mo Ibrahimu ,Bw Mo Ibrahim.
Wengine ni Mke wa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini,Mama Graca
Machel,Mfanyabiashara Tajiri,Aliko Dangote, Waziri (mdogo) wa Viwanda ,Biashara
na Uwekezaji Botswana ,Bogolo Kenewendo,Muandishi wa filamu maarufu zaidi
Duniani ya Black Panther ,Ryan Coogler Lakhdar Brahimi ,Trevor Manuel na wengine wengi.
No comments :
Post a Comment