Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa
Tigo, William Mpinga (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika
uzinduzi wa kampeni ya Tukio Kubwa Zaidi la Soka Duniani. Mashabiki wa
soka sasa wanaweza kutazama mechi za Kombe la Dunia laivu kwenye simu
zao za mkononi kupitia Star Times App na kupata dondoo muhimu za tukio
kubwa zaidi la michezo kwa kupiga *147*00# au kwenye Tigo Sports
Portal. Kulia ni Meneja wa Masoko na Matangazo wa StarTimes, David
Malisa
Meneja wa Masoko na Matangazo wa StarTimes, David Malisa
akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa
kampeni ya Tukio Kubwa Zaidi la Soka Duniani. Mashabiki wa soka sasa
wanaweza kutazama mechi za Kombe la Dunia laivu kwenye simu zao za
mkononi kupitia Star Times App na kupata dondoo muhimu za tukio kubwa
zaidi la michezo kwa kupiga *147*00# au kwenye Tigo Sports
Portal. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Tigo, William Mpinga .
Afisa wa Habari wa StarTimes,
Sam Gisayi akionesha hatu aza kujiunga na huduma mpya ya StarTimes App
itakayowezesha wapenzi wa soka kutazama mechi zote 64 za kombe la Dunia
laivu kwenye simu zao za mkononi. Hii ilikuwa katika katika uzinduzi wa
kampeni ya Tukio Kubwa Zaidi la Soka Duniani ambapo Tigo Tanzania na
StarTimes walitangaza ushirikiano huo utakaowezesha wapenzi wa soka pia
kupata dondoo muhimu za tukio kubwa zaidi la michezo kwa kujisajili
kupitia Tigo namba *147*00# au kwenye Tigo Sports Portal.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa
Tigo, William Mpinga (kushoto) akikabidhiana mpira na Meneja wa Masoko
na Matangazo wa StarTimes, David Malisa katika uzinduzi wa kampeni ya
Tukio Kubwa Zaidi la Soka Duniani. Mashabiki wa soka sasa wanaweza
kutazama mechi za Kombe la Dunia laivu kwenye simu zao za mkononi
kupitia Star Times App na kupata dondoo muhimu za tukio kubwa zaidi la
michezo kwa kupiga *147*00# au kwenye Tigo Sports Portal.
Baadhi ya viongozi na wafanyakazi
wa kampuni za Tigo Tanzania na Startimes wakiwa katika picha ya pamoja
katika uzinduzi wa kampeni ya Tukio Kubwa Zaidi la Soka Duniani jijini
Dar es Salaam.. Mashabiki wa soka sasa wanaweza kutazama mechi za Kombe
la Dunia laivu kwenye simu zao za mkononi kupitia Star Times App na
kupata dondoo muhimu za tukio kubwa zaidi la
michezo kwa kujisajili
kupitia Tigo namba *147*00# au kwenye Tigo Sports Portal.
……………………………………………………………………………
Mashabiki wa soka nchi nzima wana
sababu ya kushangilia kufuatia ushirikiano mkubwa kati ya Tigo Tanzania
na StarTimes utakaowezesha Watanzania kutazama laivu kwenye simu zao za
mkononi mechi zote za tukio kubwa zaidi la mpira wa miggu kwa mwaka
2018.
Huku joto la msimu mkubwa zaidi
wa soka kwa mwaka 2018 likizidi kupanda, kampuni inayoongoza kwa maisha
ya kidigitali ya Tigo Tanzania imetambulisha tovuti ya michezo ya www.tigosports.co.tz
itakayokuwa hewani kuanzia tarehe 14 Juni mwaka huu. Tigo pia imeungana
na mrushaji rasmi wa Kombe la Dunia, StarTimes kuzindua StarTimes
Application, itakayowezesha wapenzi wote wa soka kuwa sehemu ya
msisimko, furaha na huzuni yanayoendana na tukio hilo linalotazamwa
zaidi duniani.
‘Tigo sports portal www.tigosports.co.tz
itawezesha Watanzania kufurahia msisimko wa dakika zote tukio kubwa
zaidi la soka duniani kupitia mtandao mpana zaidi wa Tigo 4G, pamoja na
kupata habari za matukio na dondoo muhimu za tukio hilo kubwa zaidi la
mpira wa miguu duniani. Kwa kujiunga kupitia huduma iliyoboreshwa ya
*147*00#, wateja wetu pia wanaweza kushiriki katika shindano
litakalowapa nafasi ya kushinda zawadi za hadi TSH 10 milioni,’ alisema
William Mpinga, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Tigo.
Tigo inajivunia kwa mara ya
kwanza kabisa, kuwaletea mashabiki wa soka maajabu ya tukio hili kubwa
zaidi la soka moja kwa moja kwenye simu zao za mkononi. Hii inaendana na
sifa kuu ya Tigo ya kuwaelewa wateja wake na kuwapa bidhaa na huduma
bunifu zinazoboresha maisha yao ya kidigitali.
Kwa kupakua StarTimes Application
inayopatikana kupitia Applestore au Play Store, Watanzania sasa
wanaweza kuchagua bando za saa, siku, wiki au mwezi kupitia menu
iliyoboreshwa ya *147*00#. Kisha wataweza kutazama mechi zote 64 za
tukio kubwa zaidi la soka duniani kwa mwaka 2018 moja kwa moja kwenye
simu zao janja wakiwa popote nchini huku wakifurahia ubora wa hali ya
juu wa huduma za intaneti za Tigo 4G, mtandao mpana, wenye kasi ya juu
na wa uhakika zaidi nchini.
‘Teknologia yetu ya StarTimes App
inawezesha wateja wetu kuokoa gharama kubwa za intaneti, hivyo
kuwasaidia kufurahia Kombe la Dunia muda wowote na popote walipo. Hii ni
muhimu hasa ukizingatia kuwa baadhi ya mechi zinaanza saa 11 jioni,
muda ambapo wengi wetu bado tupo ofisini au njiani kuelekea majumbani.
Kwa hiyo Startimes App na Tigo intaneti zitahakikisha kuwa hukosi mechi
yoyote,’ Meneja wa Masoko na Matangazo wa StarTimes, David Malisa
alibainisha.
‘Mtandao wetu mkubwa zaidi wa
Tigo 4G unaopatikana katika miji 22 nchini, pamoja na uzinduzi wa sports
portal na ushirikiano huu na Startimes ambayo ni kampuni kubwa ya
kidigitali nchini, tutahakikisha kuwa hakuna shabiki anayepata
kisingizio cha kukosa kutazama mechi laivu, kujua matokeo na kufuatilia
dondoo mbalimblai za tukio hili kubwa zaidi la soka duniani kwa mwaka
2018,’ William Mpinga, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Tigo alimalizia.
No comments :
Post a Comment