Waziri wa Viwanda Biashara na
Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akisisitiza kuwa Serikali imejipanga
kuhakikisha kuwa kuna kiwango cha kutosha cha mafuta ya kula hapa
nchini hasa kipindi hiki cha kuelekea msimu wa mfungo mtukufu wa
Ramadhani mapema leo Bungeni Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Kilimo Dkt. Mary
Mwanjwelwa akisisistiza jambo mapema leo Bungeni Jijini Dodoma wakati wa
kipindi cha maswali na majibu.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. Anjelina Mabula akieleza juu ya faida za hati
za kimila ikiwemo kutumika kuwapatia mikopo wananchi ili waweze
kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa nchi.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji
Mhandisi Isack Kamwelwe akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na
matumizi ya Wizara hiyo leo Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard
Kalemani akieleza mkakati wa Wizara yake kuhakikisha kuwa kila kijiji
kinafikiwa na huduma ya umeme hapa nchini.
Mbunge wa Viti maalum (CCM) Mkoa
wa Kagera Mhe. Oliver Semuguruka akiuliza swali Bungeni kuhusu mikakati
ya Serikali kuimarisha sekta ya viwanda katika mkoa wa Kagera, leo
Bungeni Jijini Dodoma.
( Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO
…………….
Na: Frank Mvungi – MAELEZO, Dodoma
Serikali imesema kuwa Bilioni 59.2
zimekopeshwa na Taasisi za Fedha kwa wananchi kupitia hati za kimila
katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Akijibu swali la Mheshimiwa
Venance Mwamoto mbunge wa Kilolo (CCM) leo Bungeni, Jijini Dodoma, Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Anjelina Mabula
amesema kuwa wananchi wameweza kutumia hati za kimila kujipatia mikopo
kutoka Benki mbalimbali ikiwemo NMB PLC, CRDB PLC, Stanbic Bank, SIDO na
PSPF.
“Natoa rai kwa wananchi wote kutoa
ushirikiano katika miradi ya utoaji wa Hati za Kimila inayotekelezwa
katika maeneo yao ili ziweze kuwanufaisha kwa ustawi wa kiuchumi na
kijamii,” alisisitiza Mhe. Mabula
Akifafanua Mhe. Mabula amesema
kuwa kufikia mwezi Machi, 2018 jumla ya hatimiliki za kimila 56,506
zimeandaliwa katika maeneo mbalimbali nchini ambapo wananchi katika
maeneo hayo wamenufaika kiuchumi kutokana na mikopo waliyopata kutoka
taasisi za kifedha.
Aliongeza kuwa kuna faida nyingi
za Hati ya Kimila ikiwemo usalama wa milki, kupunguza migogoro baina ya
watumiaji wa ardhi, kutumika kama dhamana katika taasisi za fedha na
vyombo vya kisheria.
Aidha Mhe. Mabula alitoa rai kwa
wananchi wote kutoa ushirikiano katika miradi ya utoaji wa hati za
hakimiliki za kimila inayotekelezwa katika maeneo yao ili ziweze
kuwanufaisha kwa ustawi wa kiuchumi na kijamii.
Kwa mujibu wa fungu la 18, 22 hadi
47 la sheria ya Ardhi ya Vijiji Na. 5 ya mwaka 1999, hati ya hakimiliki
ya kimila ardhi kwa kuzingatia mila na desturi kwa raia wa Tanzania na
ina hadhi sawa na hakimiliki nyingine inayotolewa kisheria.
No comments :
Post a Comment