Wawakilishi wa shule za sekondari wakipokea vifaa vya michezo
vilivyotolewa na kampuni ya Coca-Cola kutoka kwa Mkuu wa Mkoa, Dkt.
Rehema Nchimbi
Mkuu wa mkoa wa singida, Dkt. Rehema Nchimbi, akifurahia zawadi ya mpira wa kufanyia mazoezi wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi, akijiandaa kupiga penati wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo.
Na Mwandishi Wetu- Singida.
Mashindano ya Copa Umisseta ngazi
ya mikoa yanaendelea ambapo yamezinduliwa mkoani Singida, katika uwanja
wa Namfua ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa mkoa huo, Dk. Rehema
Nchimbi, aliyemwakilisha Waziri wa TAMISEMI, Seleman Jafo.
Hafla ya uzinduzi huo wa michezo
hiyo ambayo inadhaminiwa na kampuni ya Coca-Cola pia
ilihudhuriwa na
viongozi mbalimbali wa serikali mkoani humo, wadau wa michezo, walimu na
wanafunzi wa shule za sekondari ambao walishiriki kucheza michezo
mbalimbali.
Mkuu wa mkoa, Dkt. Rehema Nchimbi
katika hotuba yake ya ufunguzi,aliishukuru kampuni ya Coca-Cola kwa
kutoa udhamini kwa michezo hiyo na amewaasa washiriki ambao ni wanafunzi
kuyatumia kuboresha afya na akili ili kuepuka kushiriki katika matendo
ya kihalifu kama matumizi ya madawa ya kulevya na kutojihusisha na
mapenzi kabla ya wakati.
Alisema mashindano hayo ni jukwaa
kubwa la kuibua na kuendeleza vipaji vya michezo na Ushahidi wa suala
hili upo kwa kuwa kuna wanamichezo wengi wanaotokea mkoani Singida ambao
vipaji vyao viliibuliwa na Umisseta vilevile mkoa huo katika mashindano
ya mwaka jana ulifanya vizuri katika ngazi ya kitaifa kwa kushika
nafasi ya tatu.
Kwa upande wake, Meneja Mauzo wa
bidhaa za Coca-Cola mkoani Singida, Joseph Simplis ,amesema Coca-Cola
imekuwa ikidhamini mashindano haya kwa kipindi cha miaka 3 na lengo
kubwa ni kuhakikisha inawashirikisha wanafunzi wengi zaidi nchini
sambamba na kuibua na kukuza vipaji vya michezo.Aliwaasa wanafunzi wa
Mtwara kuchangamkia fursa hii.
Katika kufanikisha michezo hii,
kampuni ya Coca-Cola imekuwa ikitoa udhamini wa vifaa vya michezo ambapo
imelenga kusambaza vifaa kwa shule za sekondari 4,000. Katika uzinduzi
huo alikabidhi vifaa vya michezo vilivyotolewa na kampuni kwa
wawakilishi wa shule mbalimbali mkoani humo.
Uzinduzi wa Copa Umisseta mkoani
Singida ni wa tano kufanyika baada ya kufanyika katika mikoa ya Dodoma,
Tanga, Mtwara na Zanzibar. Mashindano hayo ngazi ya kitaifa yatafanyika
mwezi Juni mwaka huu mkoani Mwanza.

No comments :
Post a Comment