Mnadhimu Mkuu; Luteni Jenerali
Yakubu Hassan Mohamed akizungumza wakati wa ufunguzi wa muhula wa tano
wa mashindano ya kombe la mkuu wa majeshi ya ulinzi (cdf cup 2018) jana
katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa ufunguzi
wa muhula wa tano wa mashindano ya kombe la mkuu wa majeshi ya ulinzi
(cdf cup 2018) jana katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akifuatilia matukio
mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati wa ufunguzi wa muhula wa tano wa
mashindano ya kombe la mkuu wa majeshi ya ulinzi (cdf cup 2018) jana
katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Mnadhimu
Mkuu; Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akisalimiana na mchezaji
wa Timu ya Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alipokua
akikagua timu hiyo wakati wa ufunguzi wa muhula wa tano wa mashindano ya
kombe la mkuu wa majeshi ya ulinzi (cdf cup 2018) jana katika Uwanja wa
Uhuru Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) katika picha ya
pamoja na wachezaji wa timu ya Makao Makuu ya Jeshi wakati wa ufunguzi
wa muhula wa tano wa mashindano ya kombe la mkuu wa majeshi ya ulinzi
(cdf cup 2018) jana katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam
Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM
………………………………………………………………………………..
Na: Genofeva Matemu- WHUSM
Timu za majeshi kupitia michezo
mbalimbali zimetakiwa kuweka mikakati na kuibua wanamichezo wazuri ambao
wataiwakilisha vyema nchi katika mashindano ya kimataifa na
kuleta ushindi na medali mbalimbali kama ilivyokuwa hapo zamani.
kuleta ushindi na medali mbalimbali kama ilivyokuwa hapo zamani.
Rai hiyo imetolewa na Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa
ufunguzi wa muhula wa tano wa mashindano ya kombe la mkuu wa majeshi ya
ulinzi (cdf cup 2018) katika uwanja wa uhuru jana Jijini Dar es Salaam
“Ni matarajio yangu kuwa uwepo wa
michezo hii inaashiria azma na nia thabiti ya kurejesha enzi za
majeshi yetu kutoa uwakilishi ulio mzuri katika michezo ndani na nje ya
nchi kama ilivyokuwa hapo zamani” amesema Mhe. Mwakyembe
Kwa upande wake Mnadhimu Mkuu
Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed amesema kuwa kufanyika kwa
mashindano ya kombe la mkuu wa majeshi kila mwaka kunathibitisha azma ya
JWTZ kukuza na kuendeleza sekta ya michezo nchini kwa kuunda timu za
JWTZ zitakazotumika kuimarisha timu mbalimbali za Taifa katika
mashindano ya Kimataifa.
Jenerali Yakubu amesema kuwa
uwepo wa michezo ya majeshi katika jumuiya ya Afrika Mashariki umekua
nyenzo ya kudumisha amani baina ya nchi wanachama hivyo wachezaji
watakaopata fursa kushiriki michuano hiyo washiriki vema na kuleta tija
kupitia michezo hiyo.
Mashindano ya Muula wa tano ya kombe la mkuu wa majeshi ya ulinzi (cdf cup 2018) yenye kauli mbiu isemayo “Tushiriki Michezo kama sehemu ya kazi, Kulinda Afya zetu na kudumisha mshikamano”
yataendana na uteuzi wa wanamichezo watakaoteuliwa kuunda timu za JWTZ
zitakazoshiriki mashindano tarajiwa ya Majeshi kwa nchi za Jumuiya ya
Afrika Mashariki huko nchini Kenya mwaka 2019
No comments :
Post a Comment