Msajili wa Baraza la Uuguzi na
Ukunga Tanzania, Bi. Agnes Mtawa akikaribishwa leo ofisini na watumishi
wa baraza hilo. Kushoto ni Bi. Jane Mazigo aliyekuwa akikaimu nafasi
hiyo akimpatia maua Bi. Agnes Mtawa na kulia ni Happy Masenga
anayeshughulika na mafunzo katika baraza hilo.
Bi. Mtawa akitazama zawadi ya maua aliyokabidhiwa na watumishi wa baraza hilo leo.
Msajili akiwa katika picha pamoja na watumishi wa baraza hilo leo. Kutoka kushoto ni Bi. Jane Mazigo na Bi. Happy Masenga.
……………………..
Msajili
wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agnes Mtawa leo ameanza
kazi rasmi baada ya kukabidhiwa ofisi tangu alipoteuliwa kushika nafasi
hiyo mwezi uliopita. Bi. Agnes Mtawa anachukua nafasi ya Bi. Lena
Mfalila aliyemaliza muda wake.
Awali
Bi. Mtawa alikuwa Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili (MNH) ambapo mwezi uliopita Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu alimteua kuwa Msajili
wa Baraza la Uuguzi Tanzania.
Uteuzi huo ulianza rasmi tarehe 16-04-2018 na kwamba utadumu kwa muda wa miaka mitano kuanzia tarehe ya uteuzi.
Nafasi
mbalimbali alizowahi kushika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),
Bi. Mtawa ni; Mkuu wa Mafunzo na Uajiri kuanzia mwaka 2004 hadi 2006,
Mkuu wa Mafunzo, Utafiti na Elimu kuanzia mwaka 1997 hadi 2004, amewahi
kuwa Katibu Mkuu katika baraza la uuguzi na ukunga Tanzania kuanzia
2002 hadi 2011 na mwaka 2007 aliteuliwa Mkuurugenzi wa Uuguzi katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili hadi mwezi uliopita alipoteuliwa.
No comments :
Post a Comment