*Yasema maitosita kumuondoa mwendeshaji wa sasa
SERIKALI imesema inakusudia
kuongeza mtoa huduma mwingine katika uendeshaji wa Kampuni ya Mabasi
Yaendayo Haraka (UDART) ambayeataingiza mabasi yake na kutathmini
ufanisi wa mbia wa sasa ili kuimarisha huduma ya usafiri Jijini Dar es
salaam .
Amesema iwapo itabainika kwamba
mwendeshaji wa sasa ana matatizo yaliyokithiri,
Serikali haitasita
kumuondoa na kumpa mwendeshaji mwingine kwa lengo la kuhakikisha
wananchi wanapata huduma hiyo kwa uhakika.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
ameyasema hayo leo (Alhamisi, Mei 10, 2018) wakati akijibu swali la
Mbunge wa Kinondoni, Bw.Maulid Mtulya katika kipindi cha maswali ya papo
kwa papo kwa Waziri Mkuu, Bungeni mjini Dodoma.
Katika swali lake Bw. Mtulia
alitaka kupata kauli ya Serikali juu ya uboreshaji wa wa mradi wa UDART
unaotoa huduma ya usafirishaji wa abiria Jijini Dar Es Salaam ili kuweza
kuwaondolea wananchi changamoto ya usafiri.
“Tunatafuta mbia mwingine aweze
kuingiza mabasi yake kwenye mradi huu ili aweze kuongeza ushindani na
nasi tupate kupata huduma bora kwa maana ya ushindani utaongeza huduma
bora zaidi,” amesisitiza.
Waziri Mkuu ameongeza kuwawako
wawekezaji wa ndani na nje ukiwemo Umoja wa Wamiliki wa Daladala Dar Es
Salaam (UWADAR) ambao wameonyesha nia na uwezo wa kutoa huduma hiyo na
kuufanya mradi huo kutoa huduma kwa ubora unaotakiwa.
Katika hatua nyingine, Waziri
Mkuu, amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote
nchini kuhakikisha wanasimamia vizuri suala la usafi wa mazingira katika
maeneo yao la sivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
“Mheshimiwa Spika Kupitia Bunge
lako tukufu, nawaagiza Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi pamoja na Maafisa
Afya wasimamie zoezi la usafi na kuboresha miundombinu yote na utawapima
kupitia zoezi hili,” amesema.
Amesema hayo wakati akijibu swali
la Mbunge wa Busega, Dkt. Raphael Chegeni aliyetaka kujua mkakati wa
Serikali wa kutatua tatizo la usafi wa mazingira pamoja na miundombinu
hususani katika masoko hali ya kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa
zinakusanya fedha nyingi bila kuboresha maeneo na kukithiri
kwa uchafu.
Waziri Mkuu amesema suala la
usafi limekuwa likifanyika kila jumamosi ya mwisho wa mwezi baada ya
kuasisiwa na Rais Dkt. John Magufuli, hivyo ametumia fursa hiyo
kuwaagiza watendaji hao wahakikishe maeneo yao yanakuwa safi na
miundombinu inayoweza kutumika wakati wote.
No comments :
Post a Comment