Frank Mvungi- MAELEZO
Serikali ya Awamu yaTano tangu
iingie madarakani imefanikisha Ujenzi wa Viwanda zaidi ya 3306 vikubwa
na Vidogo hadi kufikia machi 2018.
Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio
ya Mapato na Matumizi, Waziri wa Viwanda Biashara na uwekezaji, Mhe.
Charles Mwijage amesema kuwa ujenzi wa viwanda hivyo unatokana na
dhamira ya Serikali kujenga uchumi wa viwanda ili kukuza ajira na
uchumi.
“Muongozo wa Kusimamia ujenzi wa Viwanda kwa Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa umekamilika’’ Alisisitiza Mwijage
Akifafanua Mhe. Mwijage amesema
kutokana na dhamira safi ya Serikali kujenga uchumi wa Viwanda hali
iliyopelekea Tanzania kujitosheleza kwa mahitaji ya nondo, mabati,
vinjwaji na vigae.
Katika kufufua viwanda
vilivyosimama kuzalish, Mhe. Mwijage amesema kuwa msimamo wa Serikali
nikuhakikisha kiwanda cha matairi Arusha kinafanya kazi na jukumu la
kuboresha na kuendesha kiwanda hicho litakuwa mikononi mwa sekta Binafsi
huku Serikali ikibaki na hisa kulingana na rasilimali zilizopo.
Akizungumzia vipaumbele vya
Wizara kwa mwaka 2018/19 Mhe. Mwijage amesema kuwa ni kuendeleza miradi
ya kielelezo ya Mchuchuma na Liganga, Magadi soda Engaruka na Kiwanda
cha Matairi Arusha, Uendelezaji wa eneo la Viwanda TAMCO Kibaha na
mradi wa kuunganisha matrekta.
Vipaumbele Vingine ni uendelezaji
wa Mitaa, Maeneo ya Viwanda vya SIDO, Kuendeleza Kanda Kuu za
Kiuchumi, Ruvuma, Tanga, Kigoma, Manyoni, Bagamoyo, SZE na BMSEZ,
Kurasini Logistic Centre na Kigamboni Industrial Parks.
Aidha ameongeza kuwa, kati ya
Julai 2017 hadi Machi 2018 jumla ya miradi 243 yenye thamani ya dola za
kimarekani milioni 3,667 imeajiri watu 36,025 na imesajiliwa na TIC,
BRELA na EPZA.
Vilevile amesema kuwa, tangu
kuanzishwa kwa Mamlaka ya EPZ hadi mwezi machi, 2018 jumla ya mtaji dola
bilioni 1.86 uliwekezwa na mauzo ya bidhaa nje ya nchi yamefikia Dola
za Kimarekani milioni 1,359.94 na ajira 52, 698 za moja kwa moja
zimepatikana.
Kupitia mradi wa kuunganisha
matrekta ya URSUS ambapo hadi mwezi Desemba 2017, Semi knocked Down
(SKD) za matrekta 2400 yaliyoanishwa katika mkataba wa uunganishaji
unaoendelea.
Pia Wizara itaendeleza tafiti
kupitia taasisi zake za TIRDO, CAMARTEC, TEMDO, Dodoma Leather, Dodoma
SEZ na ujenzi wa Indusrial Parks.
Serikali ya Awamu ya Tano
inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli imekuwa ikisisitiza
umuhimu wa ujenzi wa uchumi wa viwanda kote nchini, Aidha Hotuba ya
makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha
2018/2019.
No comments :
Post a Comment