Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya
Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du
Toit (wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na Naibu Balozi wa Umoja wa
Ulaya (EU), Charles Stuart (wa pili kulia), Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi
ya Friedrich Ebert Stiftung Tanzania, Andreas Quasten (kushoto) pamoja
na Afisa Utawala Msaidizi na Itifaki wa ofisi za Unesco Dar es Salaam,
Rahma Islem (kulia) wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya Uhuru
wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini
Dodoma.
Mkuu
wa Wilaya ya Kongwa, Deo Ndenjembi akisalimiana na Mwakilishi wa
Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya
Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du
Toit (kulia) mara baada ya kuwasili kwenye kongamano la maadhimisho ya
Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari zinazofanyika katika Hoteli ya Morena
jijini Dodoma. Kushoto ni Afisa Utawala Msaidizi na Itifaki wa ofisi za
Unesco Dar es Salaam, Rahma Islem
Mshehereshaji
wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari,
Innocent Mungy (katikati), Mshauri wa Utawala Bora na Haki za Binadamu
wa Ubalozi wa Sweden nchini, Anette Widholm Bolme (kushoto) pamoja na
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika
(MISA-TAN), Gasirigwa Sengiyumva wakipitia ratiba ya maadhimisho hayo
yanayofanyika katika hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Mgeni
rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai
akisalimiana na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni
Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya
Unesco Nairobi, Jaco Du Toit mara baada ya kuwasili kwenye kongamano la
maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika
Hoteli ya Morena jijini Dodoma. Wengine katika picha ni Mkuu wa Wilaya
ya Kongwa, Deo Ndenjembi (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Taasisi ya
Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Salome Kitomari (wa tatu
kushoto), Afisa Utawala Msaidizi na Itifaki wa ofisi za Unesco Dar es
Salaam, Rahma Islem (wa pili kulia) pamoja na Mshehereshaji wa kongamano
hilo, Innocent Mungy (kulia).
Mgeni
rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai
(wa tatu kulia) akiongozana na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco
ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Kanda ya Afrika
Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du Toit (kulia), Mwenyekiti wa
Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Salome
Kitomari (wa pili kulia) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deo
Ndenjembi (kushoto) kuelekea kwenye mabanda ya maonyesho mara baada ya
kuwasili kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya
Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Mgeni
rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai
akipitia nakala ya gazeti la Majira huku akipata maelezo kutoka kwa
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Majira, Imma Mbuguni (wa pili kulia)
wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho kwenye kongamano la
maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika
Hoteli ya Morena jijini Dodoma. Kulia ni Meneja Usambaza wa Gazeti la
Majira, Sophia Mshangama.
Mgeni
rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai
akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mjenga Uwezo wa Mtandao wa Watetezi wa
Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Deogratius Bwire kuhusu shughuli
mbalimbali zinazofanywa na mtandao huo mara baada ya kuwasili kwenye
kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
zinazofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma. Wengine ni Mkuu wa
Wilaya ya Dodoma, Deo Ndenjembi (wa pili kushoto) na Mwenyekiti wa
Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Salome
Kitomari (wa tatu kushoto)
Mgeni
rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai
akipokea nakala ya gazeti la Mwananchi kutoka kwa wafanyakazi wa
Mwananchi Communications wakati akitembelea mabanda ya maonyesho kwenye
kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Mgeni
rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai
akipata maelezo kutoka kwa Mmoja wa Wakurugenzi na Mmiliki wa Gazeti la
Jamhuri Deodatus Balile wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya
maonyesho kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya
Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Mgeni
rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai
akipokea majarida na machapisho mbalimbali ya Umoja wa Mataifa kutoka
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella
Vuzo wakati alipotembelea banda la UN kwenye kongamano la maadhimisho ya
Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika Hoteli ya
Morena mjini Dodoma.
Afisa
Programu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Paul Mallimbo akitoa
maelezo kwa Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mh. Job Ndugai kuhusiana na kitabu cha Maadili ya Uandishi wa
Habari wakati alipokuwa akitembelea banda la Baraza la Habari Tanzania
(MCT) kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya
Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma. Kulia
ni Afisa Logistic wa Baraza hilo, Athuman Mbegu.
Mgeni
rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai
akiwasili kwenye ukumbi wa mikutano tayari kuanza kwa kongamano la
maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika
Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Mshehereshaji
wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari,
Innocent Mungy akiwakaribishwa meza kuu, wanahabari na wadau wa habari
kwenye kongamano la maadhimisho hayo yanayofanyika katika Hoteli ya
Morena jijini Dodoma.
Meza
kuu kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini
mwa Afrika (MISA-TAN), Salome Kitomari, Mgeni rasmi Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai, Mwakilishi wa
Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya
Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du
Toit pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa
Habari nchini (UTPC), Jane Mihanji.
Mgeni
rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai
akifungua kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya
Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya
Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du
Toit akitoa salamu za Unesco wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku
ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena
jijini Dodoma.
Makamu
Mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari nchini (UTPC),
Jane Mihanji akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai kufungua
kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Afisa
Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo
akizungumzia malengo ya maendeleo endelevu na jukumu la waandishi wa
habari kutumia nafasi zao kutoa taarifa kuhusu malengo hayo kwa jamii
ili yatekelezeke kwa urahisi, katika kongamano la maadhimisho ya Siku ya
Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena
jijini Dodoma.
Mtaalamu
wa Masuala ya Vyombo vya Habari na Mkufunzi wa kujitegemea, Rose Haji
Mwalimu akiongoza mjadala kuhusu mada: Wajibu wa Uongozi, Vyombo vya
Habari na Sheria katika kuhakikisha haki inatendeka na kuonekana
inatendeka wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo
vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Mwandishi
wa Habari Nguli, Ndimara Tegambwage na mwezeshaji wa mada inayohusu;
Wajibu wa Uongozi, Vyombo vya Habari na Sheria katika kuhakikisha haki
inatendeka na kuonekana inatendeka: wakati wa kongamano la maadhimisho
ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli
ya Morena jijini Dodoma.
Wakili
na Mwandishi wa Habari ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya MISA-TAN, James
Marenga akichangia mada wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya
Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Nashera
jijini Dodoma.
Mdau
wa Habari Ernest Sungura akishiriki kuchangia maoni katika mjadala
uliowasilishwa na mwandishi nguli Ndimara Tegambwage (hayupo pichani)
wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Mkuu
wa kitengo cha Mawasiliano na Habari Unesco nchini, Nancy Kaizilege
(kulia) na Mshauri wa Utawala Bora na Haki za Binadamu wa Ubalozi wa
Sweden nchini, Anette Widholm Bolme wakati wa kongamano la maadhimisho
ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli
ya Morena jijini Dodoma.
Pichani
juu na chini Sehemu ya washiriki ambao ni wahariri, waandishi wa
habari, wadau wa tasnia ya habari na wageni waalikwa waliohudhuria
kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini
yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Mgeni
rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai
katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wakiwemo wahariri, wadau
wa habari na waandishi wa habari waliohudhuria kongamano la maadhimisho
ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli
ya Morena jijini Dodoma
Mgeni
rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai
katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa habari na wafanyakazi wa
Umoja wa Mataifa, Ubalozi wa Umoja wa Ulaya pamoja na wamiliki wa vyombo
vya habari vya kijamii waliohudhuria kongamano la maadhimisho ya Siku
ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya
Morena jijini Dodoma
Mgeni
rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai
katika picha ya pamoja waandishi wa habari wakonge (Veterans)
waliohudhuria kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya
Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

No comments :
Post a Comment