Waziri wa Nishati Dkt Medard
Kalemani (wa Tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki
wengine wa Mkutano wa Kimataifa wa Japan -Africa Public Private Economic Forum unaofanyika katika Jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (wa nne kushoto) akiwa akiwa katika Mkutano wa Kimataifa wa Japan -Africa Public Private Economic Forum
unaofanyika katika Jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini.Kushoto
kwake ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi
Stella Manyanya.
……………….
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ameshiriki Mkutano wa Kimataifa wa Japan -Africa Public Private Economic Forum
katika Jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini ambao pamoja na
masuala mengine utajadili suala la uwekezaji katika Sekta ya Nishati.
Katika Mkutano huo unaofanyika
tarehe 3-4, Mei, 2018, Dkt Kalemani ameambatana na Naibu Waziri wa
Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya na maafisa
kutoka Sekta mbalimbali nchini.
Katika Mkutano huo, kampuni
mbalimbali kutoka nchini Japan zimeonesha nia ya kuwekeza nchini katika
viwanda mbalimbali ikiwemo vya kutengeneza magari aina ya Toyota.
Mkutano huo umehudhuriwa na
kampuni kubwa zaidi ya 200 kutoka nchini Japan, ambapo kampuni hizo
zitaonesha teknolojia za kisasa zinazotumika katika kutengeneza vifaa
mbalimbali vya kielektroniki na mitambo ya kuzalisha umeme.
No comments :
Post a Comment