Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Dkt.Faustine Ndugulile akizindua kanuni
za sheria ya uongozi wa hospitali za watu binafsi katika ukumbi wa LAPF
leo Jijini Dodoma.Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara hiyo Dk Otilia
Gowele na Kulia ni Msajili wa Hospitali Binafsi Dkt.Pamela Sawa.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Dkt.Faustine Ndugulile akizindua
Mwongozo wa viwango vya Msingi kwa vituo vya kutolea huduma za Afya
katika ukumbi wa LAPF leo Jijini Dodoma.Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu
Wizara hiyo Dk Otilia Gowele na Kulia ni Msajili wa Hospitali Binafsi
Dkt.Pamela Sawa.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Dkt.Faustine Ndugulile akimkabidhi
cheti cha shukrani kwa aliyekuwa mjumbe wa Bodi ya Ushauri wa Hospitali
za watu binafsi Dkt.Mohamed Ally Mohamed katika ukumbi wa LAPF leo
Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Dkt.Faustine Ndugulile akiwa katika
picha ya pamoja na wajumbe wa bodi mpya ya ushauri wa hospitali za watu
binafsi mara baada ya kuizindua leo katika ukumbi wa LAPF leo Jijini
Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Dkt.Faustine Ndugulile akizindua
Mwongozo wa viwango vya Msingi kwa vituo vya kutolea huduma za Afya
katika ukumbi wa LAPF leo Jijini Dodoma.Kushoto kwake ni Msajili wa
Hospitali Binafsi Dkt.Pamela Sawa.
Picha zote na Daudi Manongi,MAELEZO-DODOMA.
…………………
Na: Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma.
Wizara wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imezindua mfumo mpya wa TEHAMA kwa vituo
vya kutolea huduma za afya ikiwa na lengo la kuboresha utoaji wa huduma
za afya katika vituo vyote hapa nchini.
Uzinduzi huo umefanywa na Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile leo, Jijini Dodoma ambapo pia alizindua kanuni za sheria ya
uongozi wa hospitali za watu binafsi, mwongozo wa viwango vya msingi kwa
vituo vya kutolea huduma za afya nchini pamoja uzinduzi wa bodi mpya ya
ushauri wa hospitali za watu binafsi.
“Nina uhakika maombi ya usajili wa
vituo vya afya sasa yataenda kwa haraka. Waombaji watajaza fomu na
kulipia hukohuko walipo bila kufika ofisini na vile vile watakuwa na
uwezo wa kutumia mfumo kwa kutumia simu zao,” alisema Dkt. Ndugulile.
Amesema Sekta ya Afya ni miongoni
mwa sekta muhimu katika Serikali ya Awamu ya Tano ambapo sekta hiyo ni
ya tatu kwa kupata bajeti kubwa. Aidha kwa mwaka huu wa fedha jumla
ya vituo vya afya 208 vimeboreshwa kwa ajili ya kutoa huduma ya dharura
ya mama na mtoto.
Dkt. Ndugulile amesema ndani ya
bajeti hii vituo vya afya 67 vitajengwa nchini pamoja na hospitali za
rufaa kwa mikoa ambayo haina hospitali za rufaa.
Wakati huo huo, Waziri Ndugulile
ameutaka Mfuko wa Taifa wa Bima wa Afya (NHIF) kufanya majukumu
iliyopewa ikiwa ni pamoja kusajili vituo vyenye uwezo wa kutoa huduma
kutokana na vigezo vilivyowekwa na mfuko huo na kuziachia mamlaka
nyingine majukumu yake ya kukagua vituo hivyo kama vile mikataba ya
kazi ya wafanyakazi wa vituo husika.
Aidha ameutaka mfuko huo
kutafakari juu ya masharti yaliyowekwa katika kusajili vituo ambapo
kituo hakiwezi kusajiliwa mpaka kiwe katika uangalizi na mfuko huo kwa
miaka isiyopungua mitano.
Naye, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo Dkt. Otilia Gowele amesema kanuni mpya za sheria ya uongozi wa
hospitali za watu binafsi zitasaidia kusogeza huduma kwa wananchi pia
hospitali hizo kutoa huduma kulingana na mahitaji ya sasa.
No comments :
Post a Comment