Monday, April 30, 2018

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI LEO APRIL 30, 2018

1
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiwasilisha  hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Fedha kwa Wizara hiyo kwa mwaka 2018/19  Bungeni mjini Dodoma mapema leo.
2
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu akitoa maelezo Bungeni  mapema leo kuhusu mikakati ya Serikali kuhusu kufikisha umeme katika vijiji vyote hapa nchini.
3
Mbunge wa Mwanga Prof. Jumanne Maghembe akichangia hoja ya  Bajeti ya Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kuhusu mikakati inayoweza kusaidia kuendelea kukuza kiwango cha elimu hapa nchini.
4
Naibu Waziri wa  Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano  Mhe. Elias Kuandikwa akijibu swali Bungeni  mjini Dodoma kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kujenga miundo mbinu  hapa nchini.
5
Wageni mbalimbali walihudhuria Bunge wakiwemo Skauti  wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu mapema leo Bungeni mjini Dodoma.
6
Naibu  Waziri wa Fedha Dkt. Ashatu Kijaji akisisitiza jambo kwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe leo mjini Dodoma.
(Picha zote na MAELEZO

No comments :

Post a Comment