Naibu makamu mkuu wa chuo kikuu Dar es salaam, Pro. Cuthbert Kimambo akiongea na TYM wakati wa kusain makubaliano na TCCIA..
Katika
kuhakikisha Taifa letu la Tanzania linakuwa imara kiuchumi na kuwa na
nguvu kazi kubwa ya Taifa, Tanzania Chamber of Commerce Industry and
Agriculture ‘TCCIA’ imeingia makubaliano maalumu pamoja na Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam ambapo TCCIA imetiliana saini katika makubaliano hayo
‘Memorundum of Understanding’
Makubaliano
haya yanatoa nafasi kubwa kwa vijana kupitia TCCIA Youth Members,
kitengo maalumu kwa vijana hasa waliopo vyuoni kuweza kutumia rasilmali
zilizopo TCCIA kuweza kujijenga zaidi katika kazi zao pindi wanapokuwa
bado wapo shule na hata baada ya kumaliza shule.
Akizungumza
na TYM Makamu wa Rais wa TCCI Bw. Octavian Mshiu alisema TCCIA imeingia
makubaliano haya na chuo kikuu cha Dar es Salaam ili kuhakikisha inatoa
fursa kwa vijana wengi kuweza kupata nafasi za kuonesha kazi zao,
kupata nafasi ya kuwa na watu ambao watawawezesha kuweza kutimiza ndoto
zao ‘Mentorship’, kutoa nafasi ya wenye makampuni na biashara kuwatumia
vijana wa ndani ambao sio tu ni wabunifu bali pia wenye uthubutu wa
kuleta mabadiliko chanya kwenye nchi yetu, katika kuongeezea hilo prof.
Cuthbert Kimambo lisema, makubaliano haya hayataishia tu kwa chuo cha
UDSM bali wataendelea na kwenye vyuo vyote nchini
Makamu
WA Rais wa TCCIA Octavian Mshiu, wakibadilishana makubaliano Na naibu
makamu Mkuu WA chuo kikuu prof Cuthbert Kimambo baada ya kutia sain
kuhusu ushiriki wawezekaji vijana wa Chama hicho TYM.
Mkuu
wa Kitengo cha Utafiti UDSM Dr. Amelia Buriyo katika hotuba yake kwenda
kwa wanafunzi baada ya uzinduzi huu alionesha kufurahishwa na jambo
hili ambapo alitoa shime kwa vijana kuanza kuamka na kuchangamkia fursa
hii adhimu kwao kwani sio kwamba itawakutanisha na watu ambao
watawafanya ndoto zao katika miradi wanayoibuni kuwa kweli bali pia
kuwezesha kupata nyezo za kufanyia kazi hasa upatikanaji wa mikopo.
Moja
ya vijana ambao wamefanikiwa kupitia kujiajiri katika sekta ya ubunifu
wa mavazi Bw.Jeff Jersey (Speshoz) alikuwepo kwenye halfa hii ambapo
pamoja na mambo mengi aliyoyagusia alisisitiza sana kuhusiana na
kuongeza thamani kwenye kila kitu ambacho wanakifanya kwani dunia ya
sasa ni dunia ya ushindani na ushindani huhitaji sana ubunifu na
kuongeza thamni katika kila kitu ambacho tunakifanya. Bw. Speshoz ambaye
ni mkurugenzi wa kampuni ya Speshoz aliwahi kuwa mwanafunzi wa chuo
kikuu cha Dar es Salaam miaka kadhaa iliyopita.
Jeff Jersey “Speshoz” akizungumza na TYM wakati wa kusain makubaliano kati ya TCCIA na UDSM.
TCCIA Youth Members ‘TYM’ sasa imefunguliwa rasmi ambapo kila kijana anaweza kwenda kujisajili bila malipo yoyote.
No comments :
Post a Comment