Mtaalam wa ramani wa Manispaa ya Dodoma akiwaonesha wateja vilipo viwanja.
Mkuu wa Idara ya Ardhi Mipango Miji na Maliasili Joseph Mafuru (katikati) akishughulikia changamoto ya mteja.
……………………………………………………………………………..
Na Ramadhani juma, Ofisi ya mkurugenzi Dodoma
KAZI ya uuzaji wa Viwanja 10,684
imeendelea leo Jumatatu Aprili 23, 2018 katika eneo la Ofisi Kuu ya
zamani ya Manispaa zilizopo jirani na Sabasaba.
Zoezi hilo lilianza siku ya
Ijumaa Aprili 20, 2018, ambapo jumla ya wateja 399 walipatiwa
Viwanja
kwa ajili ya matumizi mbalimbali.
Katika awamu ya kwanza leo,
wateja wapatao 400 wanaotarajiwa kuhudumiwa wamepatiwa kuponi za namba
ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa kuhudumiwa.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya
Ardhi Mipango Miji na Maliasili Joseph Mafuru, zoezi la uuzaji wa
Viwanja litaendelea mpaka Viwanja vyote vitakapomalizika na kwamba
Wananchi wote wanakaribishwa.
No comments :
Post a Comment