Mkurugenzi wa Idara ya Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali na Msajili wa Mashirika hayo Bw. Marcel Katemba
akizungumza na Wasajili Wasaidizi wa Mashirka Yasiyo ya Kiserikali
kutoka katika Halmashauri na Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam katika
kikao baina yake na Wasajili Wasaidizi hao na wadau wa Mashirika Yasiyo
ya Kiserikali kilicholenga kuboresha namna bora ya uendeshaji wa
mashirika hayo mkoani humo.
Baadhi ya Wasajili Wasaidizi wa
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mkoani Dar es Salaam wakifuatilia mada na
mafunzo mbalimbali yaliyokuwa yakitolea na Msajili wa Mashirika hayo
katika kikao kilichowakutanisha kujadili namna bora ya uendeshaji wa
mashirika hayo mkoani humo kilichofanyika katika Ukumbi wa Karimjee.
Mkurugenzi Msaidizi Usajili wa
NGOs Bw. Baraka Leonard na Mkurugenzi Msaidizi Ufuatiliaji Bi. Tausi
Malima wakijadiliana jambo wakati wa kikao kazi kati ya Msajili wa
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Wasajili wasaidizi wa Mashirika hayo
mkoani Dar es Salaam kilichofanyika katika Ukumbi wa Karimjee
kilicholenga kuboresha namna bora ya uendeshaji wa mashirika hayo mkoani
humo.
Mkurugenzi wa Msaidizi Idara ya
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Leornald Baraka akiwakumbusha
washiriki mambo muhimu yanayohitaji kuzingatiwa kabla na baada ya
kusajili Shirika Lisilo la Kiserikali kwa Wasajili wasaidizi wa
Mashirika hayo kutoka katika Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam
katika kikao kilichowakutanisha Msajili wa Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali, Wasajili Wasaidizi kilichofanyika katika ukumbi wa Karimjee
kilicholenga kuboresha namna bora ya uendeshaji wa mashirika hayo mkoani
humo.
Mkurugenzi Msaidizi Ufuatiliaji
NGOs Bi. Tausi Malima akizungumza na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka
Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam na wasajili wasaidizi wa Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali mkoani humo kuhusu umuhimu wa ufuatiliaji wa
ufanyaji kazi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali baada ya kupata usajili
wake katika kikao kilichowakutanisha Msajili wa Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali na Wasajili Wasaidizi kilichofanyika katika ukumbi wa
Karimjee kilicholenga kuboresha namna bora ya uendeshaji wa mashirika
hayo mkoani humo.
Afisa Maendeleo ya Jamii na
Msajili Msaidizi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika Manispaa ya
Temeke Bw. John Bwana(kushoto)akiomba ufafanuzi zaidi kuhusu masuala
yahusuyo Usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika kikao
kilichowakutanisha Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Wasajili
Wasaidizi hao mkoani Dar es Salaam kilichofanyika katika ukumbi wa
Karimjee kilicholenga kuboresha uendeshaji wa mashirika hayo kwa
kuzingatia Sheria na miongozo mkoani humo.
Afisa Maendeleo ya Jamii na
Msajili Msaidizi wa Mashirka Yasiyo ya Kiserikali Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam Bi. Given Sure(kulia) akiuliza swali kuhusu masuala
yahusuyo Ufuatiliaji wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa Msajili wa
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini katika kikao kilichowakutanisha na
Msajili wa NGOs na Wasajili Wasaidizi mkoani Dar es Salaam kilicholenga
kuboresha uendeshaji wa mashirika hayo kwa kuzingatia Sheria na
miongozo mkoani humo.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
………………………………………………………………………………………………..
Na Anthony Ishengoma WAMJW
Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali NGOs Marcel
Katemba amewataka Wasajili Wasaidizi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali
nchini kuzisimamia NGOs ili zifanye kazi kwa kuzingatia Sheria na taratibu za nchi.
Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kazi cha Wasajili Wasaidizi ili kutoka mafunzo kwa ajili ya kukumbashana majukumu yao Kama wasajili wasaidizi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali.
Amesema kuwa kimsingi Mashirika yasiyo ya Kiserikali bado hayatambui umuhimu wenu hivyo tutawakutanisha na Mashirika haya kwa ajili kufahamiana kiutendaji na kutambuana.
Aidha Katemba amesema Mashirika yasiyo ya Kiserikali wakati mwingine yanakosa majibu muhimu kutoka kwa Wasajili Wasaidizi hivyo kusababisha waone kuwa Maafisa Maendeleo ya Jamii sio watu sahihi kusimamia shughuli zao.
“Lengo la Mafunzo haya nikukumbashana mambo muhimu ambayo yatawafanya muweze kutoa majibu stahiki kwa Mashirika haya na kuyasimamia ipasavyo baada ya kujua shughuli wanazozifanya”alisisitiza Bw. Katemba.
Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya
NGOs ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bw.
Baraka Leornard amewaambia wajumbe wa mafunzo haya kutoka Halmashauri
zote kuzisimamia NGOs ili ziweze kuhudumia Wananchi.
Bwana Baraka ameongeza kuwa kimsingi mafunzo haya ni ya
kuwajengea uwezo wasajili wasaidizi wa serikali ili waweze kujua
utaratibu wa kusajili na kuyasimamia Mashirika haya kwa matumizi mazuri
ya fedha za umma wanazopata kupitia wafadhili wao.“Pamoja na Masharika yasiyo ya Kiserikali kupata fedha kutoka kwa wafadhili ni muhimu wakatambua fedha hizo ni mali ya umma na ninyi wasajili wasaidizi mnayo haki yakujua matumizi ya fedha hizo”.Alisisitiza Bw. Baraka.
Mafunzo kama haya yamekuwa yanatolewa nchi nzima na Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali kwa Wasajili Wasaidizi wa Mashirika haya ambao ni maafisa Maendeleo wa Jamii wa Halmashauri za Wilaya hapa Nchini.
No comments :
Post a Comment