Waziri wa wizara ya
kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake
mjini Dodoma, Jumamosi 21 Aprili 2018.
Picha Zote Na Mathias Canal-WK
Waandishi
wa habari wakisikiliza kwa makini taarifa ya Waziri wa wizara ya kilimo
Mhe. Dkt Charles Tizeba ofisini kwake mjini Dodoma, Jumamosi 21 Aprili
2018.
Katibu
Mkuu wa wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akisikiliza maagizo
ya kusitisha mkatanba wa kazi wa Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania,
Leo Jumamosi 21 Aprili 2018.
Na
Mathias Canal, Wizara ya Kilimo
Waziri wa wizara ya
kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo
Mhandisi Methew Mtigumwe kusitisha mkataba wa kazi wa Mkurugenzi wa Bodi ya
Korosho Tanzania Ndg Hassan Jarufo.
Waziri Tizeba ametoa
agizo hilo kwa katibu mkuu wa wizara hiyo leo Jumamosi 21 Aprili 2018 wakati
akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Dodoma ikiwa ni muda
mchache mara baada ya kumalizika kwa dhifa ya uwekaji wa jiwe la msingi la
ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa.
Akielezea sababu za
kuagiza kusimamishwa kazi kwa mkurugenzi huyo, Mhe. Dkt Tizeba alisema kuwa
hayo yamejili baada ya kuangalia mwenendo wa Ndg Jarufo na kutafakari jinsi zao
la korosho linavyoendeshwa, ikiwa ni pamoja na kutoridhishwa na upatikanaji wa
viuwatilifu kwa wakati.
Aidha, Mkataba huo
umesitishwa kuanzia leo tarehe 21 Aprili 2018 hivyo Katibu Mkuu wa wizara hiyo
atapaswa kufanya taratibu zote za kiutumishi ikiwa ni pamoja na kumpatia
taarifa haraka muhusika na utekelezaji wake kuanza haraka.
Alisema ndani ya muda
mfupi Wizara ya kilimo itamtangaza Kaimu Mkurugenzi wa Bodi hiyo ili kuchukua
nafasi hiyo kuendeleza kusimamia sekta hiyo.
“Hizi hatua tunazochukua
ni kuhakikisha kuwa wadau wakubwa wa korosho ambao ni wakulima wanaendelea
kunufaika na zao lao, hivyo wakulima wasiwe na wasiwasi kwani pamoja na
kuondolewa Mkurugenzi huyo lakini shughuli za serikali zitaendelea kama kawaida
na maslahi yao yatasimamiwa ipasavyo” Alikaririwa Mhe. Dkt Tizeba
No comments :
Post a Comment