Na Mwandishi Maalum
Serikali ya Israel imeahidi
kuendelea kupanua wigo katika miradi yake mbalimbali iliyopo hapa nchini
ikiwemo miradi ya afya ili iweze kuwafikia wananchi wengi zaidi.
Ahadi hiyo imetolewa jana na
Waziri wa Sheria wa nchi hiyo Mhe. Aleyet Shaked alipotembelea Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ili kuona ushirikiano uliopo kati ya
Taasisi hiyo na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart –
SACH) ya nchini humo.
Mhe. Shaked alisema kuwa kwa
upande wa afya katika Taasisi ya Moyo wamekuwa wakifanya matibabu ya
moyo kwa watoto na katika siku za baadaye wataangalia namna ya kuongeza
huduma hiyo ili iweze kuwasaidia watu wengi zaidi
“Nikirudi nyumbani nitafanya
majadiliano na waziri wa Afya na kumpa mrejesho wa miradi tunayoifanya
hapa nchini, nitamuomba kuendeleza kukuza uhusiano uliopo kwa kupanua
wigo wa miradi yetu kwenye maeneo mengine ya afya katika sehemu
zingine za nchi hii itasaidia kuweza kufikia watu wengi zaidi.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi alisema kabla ya kuanzishwa kwa
Taasisi hiyo mwaka 2015 asilimia 65 ya upasuaji wa moyo kwa watoto
ulikua unafanywa na madaktari wa nje kwa kushirikiana na watanzania.
Hivi sasa madaktari wa Taasisi
hiyo wanafanya upasuaji wa moyo kwa watoto kwa asilimia 70 na asilimia
30 inafanywa kwa ushirikiano na wageni wanaokuja katika kambi maalum
za matibabu hii ni kutokana na upasuaji mwingine kuhitaji utaalam wa
juu zaidi.
“Tangu tumeanza kufanya kazi kama
Taasisi mwaka 2015 hadi sasa tumeshafanya upasuaji wa moyo kwa watoto
400 na asilimia 70 ya hao watoto wamefanyiwa na daktari wetu bingwa wa
upasuaji wa Moyo kwa watoto Godwin Sharau ambaye amesoma nchini Israel”,
alisema Prof. Janabi.
Mwaka 2015 Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete ilianza ushirikiano na SACH kwa kusomesha madaktari na
wauguzi na kufanya kambi maalum za matibabu ya moyo kwa watoto ambapo
watoto wanaokutwa na matatizo yanayohitaji matibabu ya hali ya juu
wanatibiwa nchini Israel bila malipo
No comments :
Post a Comment