Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akipokea maelezo kutoka
kwa mwakilishi wa kianda cha kutengeneza vyandarua cha (A to Z) Textile
Bw. Slyvester Kazi wakati wa maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani
ambayo kwa mwaka huu yanahadhimishwa leo Aprili 25 katika Wilaya ya
Kasulu Mkoani Kigoma.
Picha ya pamoja ikiongozwa na
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy
Mwalimu akiwa na viongozi wa Serikali na viongozi wa mashirika mbali
mbali ya kimataifa, wakiwa katika viwanja vya Umoja Wilaya ya Kasulu
mkoani Kigoma katika maadhimisho ya siku ya Malaria duniani.
Mwakilishi kutoka mradi wa
upuliziaji wa dawa ya viuatilifu ukoko majumbani Bw. Christoper Mshana,
akimpa maelekezo mgeni rasmi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu wakati wa maadhimisho ya siku
ya Malaria Duniani ambayo kwa mwaka huu yanahadhimishwa leo Aprili 25
katika Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma.
Kikundi cha ngoma kutoka Umoja
Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma kikiburudisha Viongozi na wananchi
waliofika katika viwanja vya Umoja ikiwa ni maadhimisho ya siku ya
Malaria Duniani ambayo kwa mwaka huu yanahadhimishwa leo Aprili 25
katika Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma.
Kundi la muziki wa Bongo fleva la
WEUSI wakiwa jukwaani kutoa Burudani na Elimu juu ya kinga ya ugonjwa wa
Malaria ambayo imehadhimishwa katika viwanja vya Umoja Wilaya ya Kasulu
mkoani Kigoma katika maadhimisho ya siku ya Malaria duniani.
Kundi la wananchi lililojitokeza
katika viwanja vya Umoja Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma katika
maadhimisho ya siku ya Malaria duniani ili kusikiliza ujumbe kuhusu
Malaria, mgeni rasmi wa tukio hilo ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu (MB).
……………….
NA WAMJW- KASULU KIGOMA
KIWANGO cha maabukizi ya
ugongwa wa Malaria nchini kimeshuka kwa nusu zaidi kutoka asilimia 14. 4
mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 7. 3 mwaka 2017.
Hayo yamesemwa na Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
wakati wa maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani ambayo yamefanyika leo
Wilayani Kasulu katika Mkoa wa Kigoma.
“Katika kuhakikisha
tunatokomeza kabisa ugonjwa huo Wizara ya Afya kupitia Bohari Kuu ya
Dawa (MSD) tumepokea na kusambaza vitendanishi vya malaria (mRTD) ,
vipimo 21, 428, 725, dawa za mseto dozi 12, 916, 050 kwa ajili ya
maralia isiyo kali, Sindano za kutibu Malaria kali vichupa 1, 668, 464
na vidonge vya SP dozi 6, 899, 700 kwa ajili ya tiba kinga dhidi ya
athari za malaria wakati wa ujauzito” alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa
ili watanzania tuendelee kutokomeza kabisa ugonjwa wa malaria
watanzania wanatakiwa kushiriki kikamilifu katika kutumia afua zote za
kupambana na ugonjwa huo ikiwemo kunyunyizia viuadudu vya kuua viluilui
vinavyoweza kuleta malaria.
Vilevile Waziri Ummy
amesisitiza kuwa kila Halmashauri za kila wilaya kuunda kamati
zitakazohamasisha usafi wa mazingira ili kuondoa mazalia ya mbu katika
kutokomeza malaria.
Sambamba na hilo Waziri Ummy
amezindua takwimu za ugonjwa wa Malaria nchini ambao umefanywa na
Taasisi ya Takwimu nchini NBS ambayo ndio Takwimu itayotumika na
Serikali ya Tanzania.
Kwa upande wake Waziri Wa
Elimu na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako amesema kuwa atahakikisha
wanafunzi wanapambana na ugonjwa wa Malaria kwa kuweka somo la afya kwa
shule zote za msingi na sekondari nchini.
Naye Mkuu wa Mkoa Wa Kigoma
Brigedia Jenerali Mstaafu Emamanuel Maganga ametoa wito kwa wakazi wa
kigoma kutumia vyandarua kwa matumizi sahihi na siyo kinyume na hapo
ikiwemo kufungia kuku na kuvulia samaki.
Kilele cha Maadhmisho ya
Malaria kimefikia tamati leo kwa kufanyika katika wilaya ya Kasulu
Mkoani kigoma ikiwa imebeba kauli mbiu isemayo “NIPO TAYARI KUTOKOMEZA
MALARIA WEWE JE?
No comments :
Post a Comment