Balozi
wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka H. Luvanda akimvalisha cheo cha
Brigedia Jenerali A.S Mwami ambaye ni Mwambata Jeshi wa Ubalozi wa
Tanzania nchini India.Brigedia Jenerali A.S Mwami ni miongoni mwa
Maafisa Wakuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania ambao Mheshimiwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli aliwapandisha vyeo tarehe 12 Aprili, 2018. Awali
Brigedia Jenerali Mwami alikuwa na cheo cha Kanali. Hafla hiyo fupi
imefanyika katika Ubalozi wa Tanzania nchini India na kuhudhuriwa na
watumishi wa ubalozi huo.
Brigedia Jenerali Mwami akiwa kwenye picha ya pamoja na familia yake.
Balozi Baraka Luvanda akiwa katika picha ya pamoja na Brigedia Jenerali A.S Mwami
Balozi
Luvanda pamoja na Brigedia Jenerali A.S Mwami wakiwa katika picha ya
pamoja na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini India.
No comments :
Post a Comment