Waziri wa Fedha na
Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (kulia) akiwa na mgeni wake Rais wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina, wakiingia kwenye jengo la
watu mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, baada ya
Rais huyo kuwasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kufuatia mwaliko wa
Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa kuhudhuria
Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, mjini Dodoma.
MKURUGENZI Mtendaji wa
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt.
Nyamajeje Weggoro, akizungumza jambo wakati Rais wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina (kushoto) akiwasili
kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa
ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 54 ya
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mjini Dodoma. Katikati ni Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb).
Rais wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina (kulia) na mwenyeji wake
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia)
wakigonga "tano" wakati wa mazungumzo yao wakati rais huyo
alipowasili nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa
Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa kuhudhuria
Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mjini Dodoma.
Rais wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina (kulia) akisisitiza jambo
alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es
Salaam na kupokelewa na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.
Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu kwa
mwaliko wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa
kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mjini
Dodoma. kulia ni mwenyeji wake, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.
Rais wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina (katikati) akiwasili
kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa
ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 54 ya
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mjini Dodoma. kulia ni mwenyeji wake, Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.Na Benny Mwaipaja,
WFM, Dar es Salaam
RAIS wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika-AfDB, DKT. AKINUMWI ADESINA,
ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu hapa nchini kwa mwaliko wa Rais Dkt. John
Pombe Magufuli na kuahidi kuwa benki yake itawekeza zaidi ya dola za Marekani
bilioni 1 nukta 5 kwenye sekta mbalimbali katika kipindi cha miaka miwili
ijayo,
Dkt. Adesina ameyasema
hayo alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere, Jijini Dar es Salaam, na kupokelewa na mwenyeji wake, Waziri wa Fedha
na Mipango, Dkt. Philip Mpango.
"Tunajivunia
uhusiano wetu wa muda mrefu na Tanzania ambayo ni mnufaika anayeongoza miongoni
mwa nchi za kiafrika kupata ruzuku na mikopo yenye masharti nafuu kutoka benki
yetu ambapo tangu mwaka 1971, Benki imewekeza zaidi ya dola za Marekani bilioni
3.6" alisema Dkt. Adesina
Alisema kuwa miradi
inayoendelea hivi sasa nchini Tanzania kupitia ufadhili wa Benki yake imefikia
thamani ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 2 ambapo uwekezaji mkubwa uko
katika sekta za nishati ya umeme, usafiri, miundombinu ya barabara, kilimo,
maji na usafi wa mazingira, kusaidia Bajeti Kuu ya Serikali pamoja na
uendelezaji wa rasilimali watu.
"Katika
miundombinu ya barabara peke yake, Benki yangu imewekeza zaidi ya dola za
Marekani bilioni 1.1 na kwamba uwekezaji huo utasaidia kuboresha usafirishaji
wa bidhaa na abiria hivyo kuchochea ukuaji na uendelezaji wa uchumi wa
viwanda" alisema Dkt. Adesina.
Dkt. Adesina ameutaja
mradi mwingine mkubwa wa kusafirisha umeme wenye msogo wa kilovolti 400 wenye
njia yenye urefu wa kilometa 670 katika Ukanda wa Kusini na Kusini Magharibi
mwa Tanzania, unaohusisha pia ujenzi wa vituo vya kupozea umeme katika mikoa ya
Iringa, Dodoma, Singida na Shinyanga, wenye thamani ya dola milioni 220.
"Miradi hii
pamoja na ile wa umeme wa kutumia joto ardhi pamoja na maji inayotarajiwa
kupatiwa fedha na Benki hiyo, itasaidia sana mkakati wa Mhe. Rais Dkt. John
Magufuli, ambaye ammwagia sifa kwa utendaji kazi wake mahili, wa kujenga uchumi
wa viwanda kwa kuwa na umeme wa uhakika na wenye gharama nafuu" aliongeza
Dkt. Adesina.
Alisema Tanzania
imepiga hatua katika viwango vya wananchi kupata huduma ya umeme ambapo awali
ilikuwa asilimia 18 lakini hivi sasa kiwango hicho kimepanda hadi kufikia
asilimia 38 na kwamba lengo la benki hiyo ni kutaka kiwango hicho kifikie
asilimia 82 katika miaka michache ijayo.
Alisema ili kufikia
hatua hiyo Benki yake ina mpango wa kuboresha Shirika la Ugavi wa Umeme
nchini-TANESCO ili liongeze uzalishaji wa umeme wenye gharama nafuu, kuongeza
ufanisi na kutengeneza faida ili kuchochea maendeleo ya viwanda.
Aidha, Rais huyo wa
Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, ameeleza kuwa benki yake inasiadia
kuendeleza kilimo nchini kupitia Mpango wa Kukuza Kilimo katika Ukanda Kusini
mwa Tanzania-SAGCOT, kwa kukuza masoko na uongezaji thamani ya mazao ya
wakulima yanayozalishwa kupitia mradi huo.
Akizungumzia miradi ya
kikanda, Dkt. Adesina alisema kuwa benki yake imewekeza katika miradi ya
nishati ya umeme na miundombinu ya barabara ili kuunganisha Tanzania na nchi
jirani za Burundi na Kenya ili kurahisisha biashara na kuboresha upatikanaji wa
nishati ya umeme katika nchi hizo.
Kwa upande wake,
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameeleza kuwa Benki ya
Maendeleo ya Afrika ni mshirika mkubwa wa Maendeleo wa Tanzania kutokana na
uwekezaji mkubwa uliofanywa katika nyanja mbalimbali.
Alisema kuwa AfDB,
licha ya kusaidia kwa kiasi kikubwa kufadhili miradi ya ujenzi wa barabara,
nishati na mingine mingi na mfuko mkuu wa Serikali, mwaja jana ilitoa pia mkopo
nafuu wa dola za Marekani milioni 50 kwa ajili ya kukuza mtaji wa Benki ya
Maendeleo ya Kilimo nchini-TADB, zinazotumika kukopesha wakulima.
Dkt. Mpango amesema
kuwa Rais huyo akiwa hapa nchini atatembelea mradi wa kituo cha kupooza umeme
cha Zuzu kilichoko mkoani Dodoma na ataungana na Mheshimiwa Rais Dkt. John
Pombe Magufuli kuzindua barabara ya Dodoma-Babati hadi Arusha, iliyofadhiliwa
na Benki hiyo na washirika wake.
No comments :
Post a Comment