Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiwasili kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika
Mbili wa SADC kuhusu hali ya Usalama katika Kanda, Luanda Angola.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akifuatilia kwa makini Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika
Mbili wa SADC kuhusu hali ya Usalama katika Kanda, Luanda Angola. Makamu
wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza mara baada ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika
Mbili wa SADC kuhusu hali ya Usalama katika Kanda kumalizika mjini
Luanda Angola.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa kwenye picha ya pamoja Wakuu wa Nchi na Serikali muda mfupi kabla
ya kuanza kwa Mkutano wa Troika Mbili wa SADC kuhusu hali ya Usalama
katika Kanda, Luanda Angola.
Wengine pichani kutoka kushoto ni Mheshimiwa Thomas Thabane, Waziri Mkuu wa Lesotho Mhe. Edgar Lungu, Rais wa Zambia, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Rais Joseph Kabila, Mfalme Mswati III, Mfalme wa
Swaziland Mhe. Dkt. Cyril Ramaphosa Rais wa Afrika Kusini na Mwenyekiti
wa Summit, Mhe. João Lourenço Rais wa Angola na Mwenyekiti wa Asasi ya
SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama – (SADC Organ on
Politics, Defence and Security Cooperation), Mhe. Hage Geingob Rais wa
Namibia na Makamu Mwenyekiti wa Summit (Picha na Ofisi ya Makamu wa
RaisWengine pichani kutoka kushoto ni Mheshimiwa Thomas Thabane, Waziri Mkuu wa Lesotho Mhe. Edgar Lungu, Rais wa Zambia, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Rais Joseph Kabila, Mfalme Mswati III, Mfalme wa
………………..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amemuwakilisha Mhe.
Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye
ni Mwenyekiti wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya
SADC aliyemaliza muda wake kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali
wa Troika Mbili wa SADC kuhusu hali ya Usalama katika Kanda umefanyika
hapa Luanda, leo tarehe 24 Aprili, 2018.
Mkutano huu umeitishwa baada ya
mashauriano kati ya Mheshimiwa Dkt. Cyril Ramaphosa, Rais wa Jamhuri ya
Afrika Kusini na Mwenyekiti wa SADC na Mhe. João Lourenço, Rais wa
Angola na Mwenyekiti wa Asasi ya Ushirikino ya Siasa, Ulinzi na Usalama
ya SADC
Mkutano huu umetanguliwa na kikao cha Mawaziri ambacho kilifanyika jana tarehe 23 April 2018.
Mkutano huu ulihusisha nchi wanachama sita tu wa SADC Double Troika na Viongozi wafuatao walihudhuria,
Mhe. Dkt. Cyril Ramaphosa, Rais wa
Afrika Kusini na Mwenyekiti wa Summit, Mhe. João Lourenço , Rais wa
Angola na Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na
Usalama – (SADC Organ on Politics, Defence and Security
Cooperation),Mhe. Hage Geingob, Rais wa Namibia na Makamu Mwenyekiti wa
Summit, Mhe. Edgar Lungu, Rais wa Zambia na Makamu Mwenyekiti wa SADC
Organ, Mfalme Mswati III, Mfalme wa Swaziland na Mwenyekiti wa Summit
anayetoka;
Mheshimiwa Joseph Kabila Kabange,
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Mheshimiwa Thomas Thabane,
Waziri Mkuu wa Lesotho walialikwa na walihudhuria.
Mkutano huu utapitia na kujadili ajenda zifuatazo:-
- Hali ya siasa na usalama katika Falme ya Lesotho;
- Hali ya siasa ulinzi na usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo;
- Hali ya siasa, ulinzi na usalama nchini Madagascar; na
- Masuala ya demokrasia katika kanda ( Consolidation of Democracy in the region)
KUHUSU HALI YA SIASA, ULINZI NA USALAMA NCHINI LESOHO:-
- Mkutano huu umevitaka Vyama vyote vya Siasa kulipa uzito suala la Mjadala wa Kisiasa na Mchakato wa Mageuzi ya Kisekta na kushiriki kikamilifu kwenye michakato yote ili kupata suluhisho la kudumu katika changamoto za kiusalama na kisiasa;
- Pia Mkutano huu umeitaka Serikali ya Lesotho na wadau wengine kukamilisha mjadala wa kitaifa ifikapo mwezi Juni, 2018 na kutoa taarifa kwenye kikao kijacho cha kawaida cha Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC ambacho kimepangwa kufanyika Augosti, 2018;
- Pia Misheni ya Ulinzi nchini Lesotho (SADC Preventive Mission in the Kingdom of Lesotho – SAPMIL ) imeongezewa muda kwa kipindi kingine cha miezi sita kuanzia Mei 20, 2018.
KUHUSU HALI YA SIASA, ULINZI NA USALAMA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO (DRC)
Nchi wanachama zitaombwa kuisaidia
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwenye kipindi hiki
wanachoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu kwa lengo la kuhakikisha kuwa
uchaguzi huu unafanyika katika mazingira ya amani.
Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano
huu ulitumia fursa hiyo kuomba nchi wanachama wa SADC kumuunga mkono
Mheshimiwa Stephen Maselle ( Mb), ambaye anawania nafasi ya Makamu wa
Rais wa Bunge la Afrika ( Deputy President of the Pan African
Parliament).
No comments :
Post a Comment