Balozi
wa Norway hapa nchini Mhe. Ms. Hanne-Marie Kaarstad,akimpatia Katibu
Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Mhandisi John Wiliam Kijazi zawadi ya kitabu
kinachoelezea meli ya utafiti ya Dr Fridtjof Nansen kutoka nchini Norway
iliyofanya utafiti wa uwingi wa samaki katika bahari ya Tanzania. Kulia
ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina ambaye pia alipewa kitabu
hicho. Picha na John Mapepele
Mhe.
Balozi Mhandisi John Wiliam Kijazi aliyekaa akionyeshwa namna meli ya
utafiti ya Dr Fridtjof Nansen kutoka nchini Norway inavyofanya kazi na
Kapteni wa Meli hiyo, kushoto kwake ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga
Mpina na kushoto kwake ni Waziri anayesimamia Sekta ya Uvuvi kwa upande
wa Zanzibar. Picha na John Mapepele

Mmoja
wa waongozaji meli ya utafiti ya Dr Fridtjof Nansen kutoka nchini
Norway (aliyenyoosha mikono ) akitoa maelezo wanavyoiongoza meli hiyo
kuanzia kulia Mhe. Balozi Mhandisi John Wiliam Kijazi, Mwenyekiti wa
Kamati ya Bunge Kudumu ya Kilimo Mifugo na Maji, Mheshimiwa Mahmoud
Mgimwa, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina na Katibu Mkuu wa Uvuvi
Dkt. Yohana Budeba. Picha na John Mapepele
Viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa wakiongozwa na Katibu Mkuu
Kiongozi, Mhe. Balozi Mhandisi John Wiliam Kijazi wakiingia katika meli
ya utafiti ya Dr Fridtjof Nansen kutoka nchini Norway katika Bandari ya
Dar es Salaam wakati watafiti hao walipokuja kutoa utafiti wa awali hivi

karibuni. Picha na John Mapepele.
Na John Mapepele,
Dar es Salaam
Dar es Salaam
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameitaka
Wizara ya Mifugo na Uvuvi kutumia matokeo ya utafiti wa uwingi wa
raslimali za uvuvi za bahari kuu uliofanywa na meli ya utafiti ya Dr
Fridtjof Nansen kutoka nchini Norway ili kuleta mapinduzi katika Sekta
ya Uvuvi nchini. Meli hiyo imefanya utafiti kwa ufadhili wa Shirika la
Chakula na Kilimo Duniani (FAO) kwa kushirikiana na Serikali ya
Tanzania.

Akizungumza katika Bandari ya Dar es Salam kwenye
hafla ya kuikaribisha meli hiyo baada ya kumaliza kufanya utafiti wa
siku 12 kwenye bahari ya Tanzania na kuiaga kuendelea na safari ya
utafiti, Mwakilishi wa Mheshimiwa Rais katika hafla hiyo Katibu Mkuu
Kiongozi, Mhe. Balozi Mhandisi John Wiliam Kijazi alizielekeza Wizara
na taasisi zote za Serikali kutumia tafiti zinazofanywa ili kuleta
maendeleo katika sekta husika. “Kufanya utafiti ni jambo moja na kutumia
taarifa za utafiti uliofanyika ni jambo jingine, kwa hiyo hakikisheni
mnatumia taarifa za tafiti hizi kikamilifu” alisisitiza Mhe. Balozi
Kijazi.

Aidha alitoa siku 30 kwa watafiti wa Taasisi ya Utafiti
wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) walioshiriki utafiti katika meli ya Dr
Fridtjof Nansen washirikiane na watafiti wenzao kuleta matokeo ya
utafiti huo Serikalini ili uanze kufanyiwa kazi na hatimaye kuleta tija
kwenye Sekta ya Uvuvi.

Wakati huo huo Balozi Kijazi aliishukuru
Serikali ya Norway, Shirika la Maendeleo la Norway (NORAD) na Shirika la
Chakula na Kilimo Duniani (FAO) kwa ufadhili, utaalamu pamoja na
kuisaidia Tanzania katika nyanja za sayansi za kwenye maji. “Hii ni
furaha kubwa kwa Tanzania hasa kwa kufaidika na meli yenye teknolojia ya
hali ya juu kwa upande wa utafiti wa uvuvi kutoka Serikali ya Norway na
FAO na tutafaidika zaidi tutakapopata matokeo ya utafiti kwa kujua
uwingi wa samaki, mtawanyiko wao na mazingira yake katika maji yetu”.

Alisema
utafiti huo ni matokeo ya mazungumzo yaliyofanyika Mwezi Septemba
mwaka 2017, baina ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli, alipokutana na Mkurugenzi Mkuu wa FAO Bw. Jose
Graziano da Silva, Ikulu Dar es Salaam. Alisema miongoni mwa mazungumzo
yao yalikuwa ni utafiti wa masuala ya uvuvi ili kujua kiasi na aina ya
samaki waliopo katika maji ya Tanzania. Aidha alisema ana tumaini kuwa
takwimu na taarifa za uvuvi zitakazopatikana katika matokeo ya utafiti
huu zitasaidia katika kuwavutia wawekezaji katika nyanja za uvuvi na
biashara zake kwa ujumla.

Akimkaribisha Katibu Mkuu
Kiongozi katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa
kitaifa na kimataifa, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina
alimshukuru Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kwa kumtuma Katibu Mkuu
Kiongozi kumwakilisha katika hafla hii na kumuomba kusaidia ununuzi wa
meli ya utafiti ili kufanya utafiti na kufuatilia uwingi wa rasilimali
za uvuvi bahari kuu kuwa endelevu badala ya kutegemea meli za misaada
kutoka nje ya nchi katika kufanya utafiti hapa nchini.

Waziri
Mpina alisema utafiti huo uliohusisha maji ya ndani na Ukanda wa Uchumi
wa Bahari (Exclusive Economic Zone – EEZ), na ni wa kwanza kufanyika
katika nchi yetu kwa Ukanda wa Uchumi wa Bahari, Wizara yake
itahakikisha kuwa inatumia kikamilifu taarifa za utafiti huo ili
kuongeza tija katika sekta ya uvuvi nchini. Aliiomba Serikali kusaidia
ununuzi wa meli ya doria kwenye ukanda wa bahari kuu ili kufanya doria
za mara kwa mara katika maji yetu na kulinda rasilimali za nchi.

Aidha
Waziri Mpina aliomba Serikali iwekeze zaidi katika kupambana na uvuvi
haramu na kuutangaza kuwa janga la kitaifa kwa kuwa hivi sasa taifa
linapoteza zaidi ya 75% ya thamani halisi ya pato la sekta ya uvuvi
kutokana na uvuvi haramu.

Pia Mpina alimwomba Rais kusaidia
kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) na ujenzi wa Bandari ya Uvuvi
ambayo itaongeza ajira kwa vijana, viwanda kwa ajili ya kuhifadhi na
kuchakata samaki, mauzo ya bidhaa mbalimbali kwa ajili ya meli za uvuvi
na kubwa zaidi kuinua pato la Taifa kwa ujumla. Alisisitiza kwamba,
samaki watakaovuliwa katika maji ya Tanzania watashushwa hapa nchini na
kupata takwimu halisi zitakazo ainisha samaki wanaovuliwa hapa nchini.
Aidha kwa upande wa wahisani Mpina aliwaomba waendelee kuisaidia
Serikali katika kujenga uwezo wa kufanya tafiti na watafiti wa hapa
nchini pia waendelee kushirikiana na Wizara kwenye operesheni
mbalimbali za kudhibiti uvuvi haramu.

“Tutapambana na wavuvi
haramu bila suluhu hadi kuutokomeza uvuvi haramu hapa Tanzania,
hatutoshindwa na tumedhamiria kwa dhati kufanikisha hili. Penye nia pana
njia, tumepania. Kwa heshima na taadhima ninaamini kuwa Mhe. Rais
atafanya kila awezalo kwa uwezo wake ili kuhakikisha kuwa sekta ya uvuvi
inakuwa na rasilimali za uvuvi zinasimamiwa kwa njia endelevu kwa faida
ya vizazi vya sasa na vijavyo” aliongeza Waziri Mpina.

Kwa
upande wake Balozi wa Norway hapa nchini Mhe. Ms. Hanne-Marie Kaarstad,
aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa kufanya utafiti huo na kuahidi
kuendeleza ushirikiano katika Nyanja mbalimbali. Alimuahidi Balozi
Kijazi kuwa matokeo ya utafiti huo yatawasilishwa ndani ya kipindi cha
siku 30 alizoelekeza Mhe. Balozi Kijazi.

Naye mwakilishi wa
Shirika la Chakula Duniani(FAO) hapa nchini, Fred Kafeero alisisitiza
kuwa hirika la FAO litaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania
kwenye Sekta ya Uvuvi.
Shirika la Chakula Duniani(FAO) hapa nchini, Fred Kafeero alisisitiza
kuwa hirika la FAO litaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania
kwenye Sekta ya Uvuvi.
No comments :
Post a Comment