Mtaalamu wa masuala ya Data na
Vifaa Zantel, Hamza Zuheri (kulia) akikabidhi simu aina ya Moto C kwa
mkazi wa Magomeni, Abubakar Nyakalungu Kinanda ambaye pia ni mchezaji wa
timu ya Coastal Union leo jijini Dar es salaam baada ya kuibuka mshindi
kwenye droo ya zawadi za kila siku kupitia promosheni ya ‘Jero Yako Tu’
inayoendeshwa na Zantel. Promosheni hiyo kabambe ya miezi mitatu
imelenga kuwashukuru wateja wa Zantel kwa kuwapa zawadi mbalimbali mara
wanapoongeza salio la kiasi cha shilingi 500 tu.
Mkazi wa Kigamboni, Salum Hamadi
Simai akiendesha baiskeli yake katika makao makuu ya Zantel jijini Dar
es salaam leo mara baada ya kuibuka mshindi kwenye droo ya zawadi za
kila siku kupitia promosheni ya ‘Jero Yako Tu’ inayoendeshwa na Zantel.
Kampeni hiyo kabambe ya miezi mitatu imelenga kuwashukuru wateja wa
Zantel kwa kuwapa zawadi mbalimbali mara wanapoongeza salio la kiasi cha
shilingi 500 tu. Promosheni hiyo iliyoanza Januari 15, imefanikiwa
kuwapata washindi 46 wa fedha taslim, Washindi 46 wa simu za mkononi,
Washindi 5 wa pikipiki, Baiskeli 18 na Gari 1 aina ya Sukuzi Carry mpaka
sasa.
Ofisa Mkuu wa Masuala ya Ufundi
na Teknolojia Zantel, Larry Arthur (kushoto) akikabidhi zawadi ya
baiskeli kwa mkazi wa Vingunguti, Swalahu Ibrahim leo jijini Dar es
salaam baada ya kuibuka mshindi kwenye droo ya zawadi za kila wiki
kupitia promosheni ya ‘Jero Yako Tu’ inayoendeshwa na Zantel. Kampeni
hiyo kabambe ya miezi mitatu imelenga kuwashukuru wateja wa Zantel kwa
kuwapa zawadi mbalimbali mara wanapoongeza salio la kiasi cha shilingi
500 tu.
Masoud Juma Haji ambaye ni Mkazi
wa Buguruni (kushoto) na Nadhifa Kassim Juma, mkazi wa Mburahati jijini
Dar es salaam kwa pamoja wakifurahi zawadi zao za Pikipiki walizoshinda
kwenye Promosheni ya Zantel ya Jero Yako Tu ambapo walikabidhiwa leo
jijini Dar es salaam. Promosheni hiyo kabambe ya miezi mitatu imelenga
kuwashukuru wateja wa Zantel kwa kuwapa zawadi mbalimbali mara
wanapoongeza salio la kiasi cha shilingi 500 tu.
Masoud Juma Haji ambaye ni Mkazi
wa Buguruni akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam
baada ya kuibuka mshindi wa Pikipiki kwenye droo ya wiki katika
Promosheni ya Jero Yako Tu inayoendeshwa na Zantel. Promosheni hiyo
kabambe ya miezi mitatu imelenga kuwashukuru wateja wa Zantel kwa kuwapa
zawadi mbalimbali mara wanapoongeza salio la kiasi cha shilingi 500
tu.
Mwakilishi wa Milicom-Afrika,
Wane Ngambi (kulia) akikabidhi ufunguo wa gari kwa Twaha Abdallah Seif
ambaye ni Mkazi wa Kinondoni na mshindi wa zawadi kuu kwenye droo ya
kwanza ya Mwezi ya promosheni ya Zantel ya Jero Yako Tu katika hafla
ambayo imefanyika leo jijini Dar es Salaam
Mwakilishi wa Milicom-Afrika,
Wane Ngambi (kulia) akimpongeza Bwana Twaha Abdallah Seif ambaye ni
Mkazi wa Kinondoni na mshindi wa zawadi kuu kwenye droo ya kwanza ya
Mwezi ya promosheni ya Zantel ya Jero Yako Tu katika hafla iliyofanyika
leo jijini Dar es salaam.
ZANTEL leo imekabidhi gari aina
ya Toyota Suzuki Carry kwa mshindi wa kwanza wa zawadi kuu baada ya
mshindi huyo kushiriki kikamilifu kwenye kampeni inayoendelea ya Kampuni
hiyo ya ‘Jero yako tu’.
Hafla ya utoaji wa zawadi hiyo
kubwa imefanyika katika ofisi za makao makuu ya Zantel jijini Dar es
Salaam ambapo ilimshuhudia ndugu Mohammed Twaha (40) mfanyabiashara na
mkazi wa Kinondoni akiondoka na zawadi ya kwanza kubwa katika kampeni
hiyo.
Pamoja na zawadi hiyo kuu kwa
mshindi huyo, wengine waliojinyakulia zawadi kabambe ni
pamoja na ndugu
Masoud Juma Haji ambaye alishinda pikipiki, na Swalahu Ibrahim, Rashid
Suleiman Rashid na Salum Hamadi Simai ambao waliojishindia zawadi ya
baiskeli katika kundi la zawadi za kila wiki. Wengine walikuwa Nyakungu
Kinanda na Juzza Moiz ambao wote walishinda smartphone ya Moto C 4G.
Akizungumza wakati wa hafla ya
utoaji wa zawadi hizo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Sherif El Barbary
alisema, “Tunafurahi kukabidhi zawadi yetu kubwa ya kwanza na tuna imani
kwamba itawahamasisha wateja wengine wa Zantel kuendelea kushiriki
katika promosheni hii ili waweze kuibuka na ushindi. Itakuwa ni fahari
kubwa kuona sura mpya zaidi za watumiaji wa mtandao wa Zantel
wakijishindia zawadi mbalimbali kama hawa wenzao. “
El-Barbary alibainisha kwamba
Suzuki Carry hutumiwa zaidi kwa biashara hapa nchini Tanzania na kwamba
utafiti mdogo ambao wameufanya umebaini kuwa wamiliki hupata pesa nzuri,
na takwimu ya harakaraka inaonyesha wamiliki hao huingiza kati ya
25,000 / – 30,000 / – kwa siku na kupata karibu 900,000 / – kwa mwezi
ambayo ni takriban 10.8m/ – kwa mwaka.
Alisema Zantel pia itasaidia
gharama za usajili, leseni ya barabara na bima ya mwaka mzima kwa
washindi wake wote wa vyombo vya moto.
Kwa upande wake, Mtaalamu wa
Idara ya Data na Vifaa Zantel, Bwana Hamza Zuheri alisema, tangu
promosheni ilipoanza Januari 15, wamefanikiwa kuwapata washindi 46 wa
fedha taslim, Washindi 46 wa simu za mkononi, Washindi 5 wa pikipiki,
Baiskeli 18 na Gari 1 aina ya Sukuzi Carry mpaka sasa.
Kwa mujibu wa Zuheri, alisema
lengo la promosheni ya ‘JERO YAKO TU’ inalenga kutoa zawadi na
kuwashukuru wateja wa Zantel baada ya mafanikio ya marekebisho ya
mtandao mpya wa kisasa na kuzindua mfumo wa 4G takribani katika mikoa 22
nchini Tanzania.
“Hatuoni njia yoyote nzuri ya
kusherehekea mafanikio haya zaidi ya kufanya hivyo na watu ambao
wametufikisha hapa, hususan wateja wetu waaminifu,” alisema Zuheri.
Aliwakumbusha wateja wanaoshiriki
katika promosheni hii kuwa ni rahisi sana, wanachopaswa kufanya ni
kununua muda wa maongezi wa kiwango cha kuanzia Sh.500 na moja kwa moja
wataingia kwenye droo. Hata hivyo, aliongeza kuwa, ili kujiwekea nafasi
ya kushinda zawadi kubwa, mteja anatakiwa kushiriki mara nyingi zaidi.
Aliongeza kuwa zawadi za
promosheni ni kuanzia simu za 4G na pesa taslimu 50,000 ambazo
zinashindaniwa kila siku, pikipiki na baiskeli 4 ambazo zinashindaniwa
kila wiki na Toyota Suzuki Carry ambayo ni zawadi kuu inayoshindaniwa
kila mwezi.
ZANTEL daima imedhamiria kuwaweka
wateja wake mbele kwa kuwapa teknolojia za kisasa pamoja na ubora wa
mtandao wa kuaminika na kuwa mtandao bora unaotoa huduma za data nchini.
No comments :
Post a Comment