Katibu Tawala Mkoa wa Dar es
Salaam Bi. Theresia Mbando akifungua kikao cha Tathmini ya Utekelezaji
wa Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Da r es salaam kw niaba ya Katibu
Mkuu OR-TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe.
Msimamizi Kiongozi wa Mradi wa
Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam kutoka Benki ya Dunia Ndg. Erick
Dickson akitoa maelekezo kwa washiriki wa kikao cha tathmini ya
utekelezaji wa Jiji la Dar es salaam.
Wasimamizi wa Mradi wa
Uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam wakifuatilia kwa makini
uwasilishaji wa mada mbalimbali katika kikao cha Tathmini ya Utekelezaji
wa Mradi wa Dmdp.
Katika Picha ya Pamoja na Katibu Tawala Mkoa wa Dar es salaam Bi.Theresia Mbando }katikati} akiwa na Msimamizi Kiongozi wa DMDP
kutoka Benki ya Dunia Ndg. Erick Dickson pili}kushoto}, Mkurugenzi wa
Idaya ya Uendelezaji Miji OR-TAMISEMI Ndg. Mkuki Hante}Kwanza kushoto}
pamoja na Mratibu Msimamizi wa miradi inayotekelezwa na Beni ya Dunia
chini ya OR-TAMISEMI Ndg.Davis Shemangali.
…………………………………………………………………………..
Nteghenjwa Hosseah,OR-TAMISEMI.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Mussa Iyombe amewataka washiriki
wa kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la
Dar es Salaam “DMDP” kuwa makini katika kuchambua taarifa mbalimbali za mradi zitakazowasilishwa katika kikao hicho.
Akisoma hotuba kwa niaba ya
Katibu Mkuu katika kikao hicho Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam
Bi. Theresia Mbando amesema kuwa tathmini hii inayofanyika kwa sasa
itasaidia kutambua kwa upana wake huku ikilenga vipengelea vyote vine
ambavyo vimelengwa
kutekelezwa katika mradi huu.
“Mradi huu Mkubwa wenye lengo la
kuboresha Jiji la Dar es salaam ili lizidi kuwa bora katika Sekta ya
miundombinu, usafiri mjini, usalama, makazi bora sambamba na kujenga
uwezo wa Kitaasisi pamoja na mifumo stahiki na ya kutosha kutunza
kumbukumbu na takwimu itakayosaidia katika Ukusanyaji wa mapato ndio
ambao tunajadili hapa leo kuangalia namna wataalamu wetu walivyusimamia
na nini kimefanyika kwa kiasi gani na kwa kiwango gani” alisema
Bi.Mbando.
Aidha Bi. Mbando aliongeza kuwa
tunategemea mawazo yenu, hoja zenu za msingi katika kujenga na kuboresha
mipango iliyopo ya Utekelezaji wa mradi huu, ninyi kupitia Kikao hiki
mtaboresha mipango iliyopo, mtatukosoa, mrarekebisha na mtatoa mwanga wa
njia gani sahihi na bora ya kufuata ili mradi uweze kutekelezwa kwa
mafaniko makubwa na kutatua shida za wananchi.
katika Kikao hicho mwakilishi wa
Benki ya Dunia ambaye pia ndiye Msimamizi Kiongozi wa Mradi wa
Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam kutoka Benki ya Dunia Ndg. Erick
Dickson amesema Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia
wameleta Mradi utakaobadilisha muonekano wa Jiji la Dar es Salaam.
Aliongeza kuwa tunatakiwa
kuangalia kwa Makini namna ambavyo mradi huu unavyotekelezwa katika
kipindi hiki cha Nusu Mwaka; Yale yaliyopangwa yametekelezwa, malengo ya
mradi yamefikiwa,Wananchi wamenufaikaje kupitia mradi huuna je hakuna
athari zozote za kimazingira zilizotokea bila kusahau ushiriki wa
wananchi upo kwa kiasi gani.
Katika awamu ya kwanza ya mradi
huu ambayo inatekelezwa kwa kipindi cha 2016 -2020 Mradi utagharimu
jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 300 ambazo ni Fedha za mradi ambazo
ni Fedha za Mkopo kutoka Benki ya Dunia. Aidha Shirika la maendeleo la
Nchi za Nordic litatoa ruzuku ya dola za kimarekani milioni Tano kwa
ajili ya kukabili changamoto za mabadiliko ya Tabia ya Nchi
Wakati huo huo Serikali ya
Uingereza kupitia Shirika la maendeleo la DFID linachangia ruzuku ya
Paundi 25 milioni kwa ajili ya kuboresha Bonde la Mto Msimbazi na
Serikali ya Tanzania inachangia dola za kimarekani milioni 25 kwa ajili
ya ulipaji wa fidia kwa wananchi wanaoathirika na mradi.
Kikao hiki cha Siku tatu
kinahusisha wataalamu kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi, Wasimamizi wa
mradi kutoka Benki ya Dunia, Wataalam kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa
Dar es salaam pamoja na washauri wa mradi kutoka kampuni mbalimbali
zinazofanya kazi za mradi huu.
No comments :
Post a Comment