Na Paschal Dotto-MAELEZO
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma
(UDOM) Rais Mstaafu (Awamu ya Tatu), Mhe. Benjamin William Mkapa
ametangaza uteuzi wa Profesa Egid Beatus Mubofu kuwa Makamu Mkuu wa
Chuo Kikuu hicho, nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Profesa Idris
Suleiman Kikula.
Uteuzi huo umetangazwa rasmi leo
tarehe 5, Machi 2018 kupitia taarifa iliyotolewa kwa
vyombo vya habari
na ofisi ya Mkuu wa UDOM, Mhe. Benjamin Mkapa.
Kabla ya uteuzi huo Profesa Mubofu
alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), na kabla
ya hapo alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM).
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi wa Profesa Mubofu unaanza rasmi tarehe 17 Machi, 2018.
Profesa Idris Kikula ni miongoni
mwa wanazuoni waandamizi wanaoheshimika ndani na nje ya nchi kitaaluma
kwa kushiriki katika tafiti mbalimbali za kisayansi na kijamii
Ameshiriki katika tafiti hizo kwa
kushirikiana na taasisi nguli za kitafiti hapa nchini kama REPOA,
pamoja na taasisi ya UONGOZI.
UDOM ndio chuo kikuu pekee chenye
uwezo mkubwa wa kuchukua wanafunzi wengi hapa nchini na Afrika Kusini
mwa jangwa la Sahara na inakadiriwa kina uwezo wa kuchukua wanafunzi
takriban 40,000, pia kina eneo la ukubwa wa hekari zaidi ya 6000
No comments :
Post a Comment