Waziri wa
Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akihutubia wajumbe wa Kamati
za Kudumu za Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na
Mazingira wakati akifungua warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara
yake mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa kuhusu mradi wa SECO
ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini
kupitia sekta ya Utalii nchini.
Na Hamza Temba, Dodoma
………………………… ……………………….
…………………………
Wizara ya Maliasili na Utalii imeendesha warsha ya siku
moja ya kuwajengea uelewa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Ardhi,
Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu mradi wa
SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini
kupitia sekta ya Utalii nchini.
Akifungua warsha hiyo ya siku moja iliyofanyika mjini
hapa jana, Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Hamisi Kigwangalla alisema lengo
la warsha hiyo ni kuwajengea uelewa wajumbe hao kuhusu utekelezaji na
mafanikio ya mradi huo unaofadhiliwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya
Tanzania na nchi ya Uswizi kupitia shirika la kiuchumi la State
Secretariat for Economic Affairs-SECO.
Alisema mradi huo pia unalenga kuongeza ununuzi wa mazao
na bidhaa za mbogamboga na matunda zinazozalishwa Tanzania, kuongeza
ajira kwa Watanzania waliojifunza vema masuala ya utalii, na kuongeza
nafasi ya kujadili dhana ya Utalii Wenye Manufaa kwa jamii.
“Mradi huu unaratibiwa na Wizara ya Viwanda, Biashara na
Uwekezaji na kutekelezwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, Taasisi za
Umoja wa Mataifa zinazohusika na eneo la Maendeleo ya Biashara (UN
Trade Cluster Organizations) – UNIDO, UNCTAD, ITC na ILO, taasisi za
Serikali na zisizo za Serikali, na sekta binafsi” alisema Dk.
Kigwangalla.
Alisema awamu ya kwanza ya mradi huo ilitekelezwa
kuanzia mwaka 2014 hadi 2016 ambapo jumla ya Dola za Kimarekani milioni
3.5 zilitumika.
“Awamu ya pili ya mradi ilianza kutekelezwa mwaka 2017
na utarajiwa kukamilika mwaka huu 2018. Jumla ya Dola za Kimarekani
milioni 1.9 zimetumika katika awamu hii ya mradi” alisema.
Alisema mradi huo umekuwa na mafanikio makubwa katika
kuwawezesha wananchi kiuchumi na kuhifadhi mazingira, na kufanya utafiti
wa mazao mbalimbali ya utalii ambao utawezesha kuandaa Sera na Mikakati
mipya ya kukuza Utalii hapa nchini.
Warsha hiyo ya siku moja imehudhuriwa pia na Naibu
Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina
Mabula ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,
Maliasili na Utalii.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla
akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii wa Wiazara hiyo,
Degracious Mdamu muda mfupi kabla ya kufungua warsha ya siku moja
iliyoandaliwa na Wizara yake mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa
wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Ardhi, Maliasili na Utalii na
Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga
kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya
Utalii nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii, Ernest
Mwamaja ambaye aliwasilisha mada katika warsha hiyo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla
akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge Ardhi,
Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira muda mfupi kabla
ya kufungua warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara yake mjini
Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa kuhusu mradi wa SECO ambao
unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia
sekta ya Utalii nchini.
Baadhi ya
wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na
Viwanda, Biashara na Mazingira wakifuatilia moja ya mada iliyowasilishwa
katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara Maliasili na Utalii
mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe hao kuhusu mradi wa
SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini
kupitia sekta ya Utalii nchini.
Naibu Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula ambaye pia ni
mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii
akichangia moja ya mada iliyowasilishwa katika warsha ya siku moja
iliyoandaliwa na Wizara Maliasili na Utalii mjini Dodoma kwa ajili ya
kuwajengea uelewa wajumbe wa kamati hiyo na kamati ya Viwanda, Biashara
na Mazingira kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya
wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili
na Utalii, Deograsious Mdamu akitambulisha wajumbe wa meza kuu wakati wa
warsha hiyo.
Baadhi ya wajumbe wa kamati hizo wakifuatia moja ya mada
iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Masoko kutoka Bodi ya
Utalii Tanzania, Ernest Mwamaja (hayuko pichani)
Baadhi ya wajumbe wa kamati hizo wakifuatia moja ya mada
iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Masoko kutoka Bodi ya
Utalii Tanzania, Ernest Mwamaja (hayuko pichani)
Baadhi ya washiriki na wawezeshaji wa warsha hiyo kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.

No comments :
Post a Comment