Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Japhet Hasunga akikagua gwaride la Maafisa wa Misitu na
Wanyamapori 108 kutoka Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) na
Mamlaka ya Eneo la Ngorongoro muda mfupi kabla ya kuwatunuku vyeti vya
kuhitimu mafunzo ya Jeshi Usu katika kituo cha Mlele mkoani Katavi.
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Japhet Hasunga (wa tano kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na
viongozi, Maafisa wa Misitu na Wanyamapori 108 kutoka Wakala wa huduma
za Misitu Tanzania (TFS) na Mamlaka ya Eneo la Ngorongoro muda mfupi
baada ya kuwatunuku vyeti vya kuhitimu mafunzo ya Jeshi Usu jana katika
kituo cha Mlele mkoani Katavi.
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Japhet Hasunga (wa pili kushoto ) akimkabidhi cheti cha kuhitimu
mafunzo ya jeshi Usu, Mkurugenzi wa Mipango na Matumizi Endelevu ya
Rasilimali za Misitu za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)
Mohamed Kilongo katika kituo cha Mlele mkoani Katavi. Wa kwanza
kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Lilian Matangi, wa kwanza kulia ni
Mtendaji Mkuu wa TFS, Prof, Dos Santos Silayo pamoja na Tutubi
Mangazeni.
Baadhi ya Maafisa wa Misitu na
Wanyamapori 108 kutoka Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) na
Mamlaka ya Eneo la Ngorongoro wakimsikiliza, Naibu Waziri Japhet
Hasunga muda mfupi kabla ya kutunukiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo ya
Jeshi Usu jana katika kituo cha Mlele mkoani Katavi.
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na wahitimu wa Jeshi Usu wakati wa
kuhitimisha mafunzo hayo jana mkoani Katavi
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akipokea salamu za Jeshi Usu wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo.
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akiwa na baadhi ya viongozi
wakifurahia ulengaji wa shabaha ulioneshwa na baadhi ya wahitimu wa
mafunzo hayo jana katika kituo cha cha Mlele mkoani Katavi.
Baadhi ya Maafisa wa Misitu na
Wanyamapori 108 kutoka Wakala wa hudum za Misitu Tanzania (TFS) na
Mamlaka ya Eneo la Ngorongoro wakila kiapo muda mfupi kabla ya
kutunukiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo ya Jeshi Usu jana katika kituo cha
Mlele mkoani Katavi.
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Japhet Hasunga ( wa pili kulia) akiwa na baadhi ya viongozi
wakifurahia jambo kabla ya kuagana katika uwanja mdogo wa ndege uliopo
katika kituo cha Mlele mkoani Katavi.
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Japhet Hasunga (katikati ) akiwa kwenye picha ya pamoja
menejimenti ya Wakala wa hudumza za Misitu Tanzania (TFS) mara baada
ya kuwatunuku vyeti vya kuhitimu mafunzo ya Jeshi Usu jana katika kituo
cha Mlele mkoani Katavi.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Tutubi Mangazeni akizungumza na Maafisa wa Misitu na
Wanyamapori 108 kutoka Wakala wa hudum za Misitu Tanzania (TFS) na
Mamlaka ya Eneo la Ngorongoro muda mfupi kabla ya kutunukiwa vyeti vya
kuhitimu mafunzo ya Jeshi Usu jana katika kituo cha Mlele mkoani Katavi
PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA- MNRT
…………………….
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Japhet Hasunga amewaagiza wahifadhi wote nchini kuhakikisha
kuwa hakuna misitu inayoendelea kuharibiwa ikiwa ni pamoja na
kuimarisha utoaji wa elimu kwa wananchi wanaozunguka misitu ya hifadhi
ili wasiweze kukata miti ovyo kwa ajili ya makazi na shughuli za kilimo
Ametoa agizo hilo jana Machi,
24, 2018 katika Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi wakati akifunga mafunzo ya
kwanza kwa Wakala ya Huduma za Misitu (TFS) ya mabadiliko ya
kuelekea
mfumo wa Jeshi Usu kwa Maafisa na viongozi 108 wa TFS na Mamlaka ya
Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro.
“Misitu yetu inaendelea
kuharibiwa kutokana na baadhi ya watu kuendesha shughuli za kibinadamu
katika maeneo ya hifadhi kama vile uchimbaji madini usiozingati
taratibu, uchomaji misitu kwa ajili ya kuandaa mashamba pamoja na kilimo
cha kuhama hama.’’Kazi ya ulinzi wa rasilimali zetu za asili ni yetu na
tusikubali hali hii iweze kuendelea,,” alisema Waziri Hasunga
Aidha, alitoa wito kwa
wananchi wote kuendelea kuheshimu Sheria za nchi na kuacha kufanya
shughuli za kibinadamu kwenye maeneo ya hifadhi ikiwemo kuingiza mifugo,
kuanzisha kilimo, makazi na ukataji wa miti kwa ajili ya kuchoma mkaa
na matumizi mengineyo.
Awali akizungumzia mafunzo
hayo alisema, lengo ni kubadilisha utendaji katika sekta ya uhifadhi
kutoka ule wa kiraia kwenda wa jeshi usu ambao utaongeza nidhamu,
uwajibikaji, uadilifu na maadili kwa watumishi wote wa sekta hiyo ili
waweze kusimamia ipasavyo uhifadhi endelevu wa maliasili za taifa.
Alisema katika kuelekea mfumo
huo, Jeshi hilo litakuwa moja hali itakayosaidia watumishi wote
kuzungumza lugha moja bila kujali kada anayoitumikia. Sheria ya
Wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009 inampa Waziri mamlaka ya kuunda Jeshi
Usu.
Alisema mfumo huo wa Jeshi Usu
baada ya mchakato wake kukamilika utakuwa na mnyororo mmoja wa mamlaka
(chain of comand) na kwamba utahusisha taasisi zote za uhifadhi
zilizopo chini ya wizara yake kwenye sekta ya wanyamapori, misitu na
mali kale. “Kutakuwa na utaratibu kama majeshi mengine yanavyofanya,
kama unataka kupanda cheo lazima uhudhurie mafunzo mengine zaidi ya haya
” alisema.
Akizungumzia mafanikio ya vita
dhidi ya ujangili na matunda ya mafunzo hayo alisema, “Katika siku za
hivi karibuni tumepiga hatua kubwa ya kupambana na usafirishaji magogo
nje ya nchi kwa kuimarisha ulinzi katika bandari , Kwa dhati napongeza
jitihada zinazofanywa na zinazoendelea kufanywa na wahifadhi, maaskari
watumishi wengine na wadau wetu wote kwa ujumla ambazo zimeimarisha hali
ya uhifadhi wa maliasili zetu”.
Alisema kwa kiasi kikubwa
matukio ya uharibifu wa misitu pamoja na usafirishaji wa magogo
imepungua na kwamba hata zile bandari bubu zimethibiwa kwa kiasi kikubwa
hali inayopelekea majangili kuachana na kazi hiyo ili kukimbia mikono
ya sheria.
Naye, Mwakilishi wa Mkuu wa
Mkoa wa Katavi, Lilian Matinga alimuomba Naibu Waziri huyo kuona
uwezekano wa Maafisa Maliasili pamoja na maafisa nyuki wa Halmashauri
zote nchini nao washirikishwe katika mafunzo hayo kwa vile wote jukumu
lao ni moja ambalo ni kulinda na kuendelea uhifadhi wa maliasili.
Kwa upande wake Mwakilishi wa
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Tutubi Mangazeni akitoa nasaha zake kwa
wahitimu wa mafunzo hayo ya Jeshi Usu, aliwataka wawe mfano wa kuigwa
katika kutenda kazi uhifadhi, maadili mema na nidhamu
Naye, Mtendaji Mkuu wa Wakala
wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) alisema licha ya Taasisi yake
kushiriki katika mafunzo hayo, inaangalia uwezekano wa kuanza kutumia
satellite pamoja na ndege zisizo na rubani ili kupunguza gharama za
kufanya doria kwa kutumia magari.
Mhifadhi Elizabeth Malya
ambaye ni mhitimu wa magfunzo hayo kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro alisema mafunzo hayo yamewafanya wawe wazalendo zaidi kwa
kutii amri na kutekeleza maagizo ya walio juu yao.
Mafunzo hayo ya wiki nne
ambayo yalianza Februari, 24 mwaka huu yalihusisha Wakurugenzi , Wakuu
wa vitengo kutoka Makao makuu ya TFS, Wakuu wa Misitu ya Hifadhi,
Maafisa Wanyamapori kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro.
Mafunzo hayo yalihusisha
matumizi sahihi ya silaha, mbinu mbalimbali za kupambana na uhalifu,
huduma ya kwanza, ukakamavu, sheria mbalimbali zinazosimamia maliasili,
ukamataji na upekuzi wa wahalifu na jinsi ya kuwafungulia hati za
mashtaka.
No comments :
Post a Comment