NA MWANDISHI WETU
SISI
ni wakazi wa Kata tano za Wilaya ya Kinondoni za Bunju, Makongo, Mbezi
Juu, Mabwepande na Wazo. Sisi ni wananchi ambao tayari tulikwisha
athiriwa na mradi wa bomba la maji la Ruvu Juu ambapo wakati wakipitisha
mradi huo tulitakiwa kupisha mita tano kutoka katika mradi huo na
tukatekeleza.
Hivi
sasa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasa) imetoa
notisi na kututaka tuondoke ndani ya mita 15 kutoka katika mradi wa
bomba hilo jambo ambalo sio sheria, kwani sheria iliyopo inataka
wanaopaswa kuondoka ni wale walio ndani ya mita 5.
Sisis
wananchi tumeshangazwa na kusikitishwa na matamko yanayotolewa na
Dawasa kwani ni wazi wanataka kutumia mabavu kutuondoa katika maeneo
yetu.
Awali
ulipoanza kutekelezwa mradi huo hatukupinga ndiyo maana wale waliokuwa
ndani ya mita tano waliamua kuondoa na kuvunja nyumba zao kupisha mradi
huo ambao umeshatekelezwa na kuanza kazi kwa kipindi cha miaka mitatu
hadi sasa.
Kutokana
na kushindwa kuelewana na Dawasa tumelazimika kukifikisha kilio chetu
kwa Rais wetu mpendwa John Magufuli tunatambua kuwa busara na hekima
aliyojaliwa na Muumba anaweza kutupatia ufumbuzi wa suala hili.
Hivi
sasa hatuwezi kuishi kwa amani kutokana na muda wote kuwaza mahali pa
kwenda iwapo Dawasa wataamua kutuvunjia nyumba zetu. Wengine ni wajane
tuna familia zinazotuangalia hivyo kama tutabomolewa nyumba zetu hakika
hakuna msaada mwingine utakaotuokoa.
Tunasema
kweli kuwa msaada wetu uliobaki ni Rais Magufuli ambaye amekuwa
mkombozi wa kutatua kero nyingi za watu wa chini kama sisi
zinazozotukabili.
Rais
Magufuli anavyowajali wanyonge ndiyo maana tumelazimika kufikisha kilio
hicho kwake ili aweze kuwasaidia tusiweze kuondolewa katika maeneo haya
ambayo ndiyo mkombozi wetu hatuna pengine pa kwenda.
Sisi
ni wakazi wa Kata tano za wilaya ya Kinondoni, tunachoshangaza ni kuona
Dawasa ikitunyima amani sisi tulioko katika Kata hizo wakati bomba hilo
limepita katika maeneo mbalimbali ya wilaya hii.
Tunachojiuliza Mhe Rais Magufuli ni kwanini manyanyaso haya yanafanywa kwetu tu? Na sio maeneo mengine yanayopita bomba hilo?
Pia
kinachotushangaza mradi huo umekwisha tekelezwa na unafanyakazi sasa
hivyo kuna sababu zipi za Dawasa kutaka tuvunje nyumba zetu wakati mradi
umeshafanyika?
Mhe
Rais Magufuli maeneo haya kuna miradi mbalimbali zikiwemo shule ambazo
zimekuwa zikipokea watoto wasio na uwezo na kusomeshwa bure, wapo yatima
pia wanasomeshwa bure katika shule hizo hivyo iwapo Dawasa watabomoa
miradi ya shule hizo ni uhakika kuwa watoto waliopo katika shule hizo
watakosa masomo.
Rais
Magufuli sisi wananchi tunachotambua kuwa Mamlaka hiyo inapaswa kubomoa
nyumba zilizo katika mita tano kushoto na kulia kama sheria ya mwaka
2001 ilivyoagiza na sio vingine.
Tunakuomba
Rais Magufuli uingilie kati suala hilo ili haki iweze kutendeka kwetu
sisi wananchi wa chini kwani kama Dawasa inahitaji kupata ardhi zaidi
kwa ajili ya mradi huo basi wanachopaswa kufanya ni kufuata sheria ikiwa
ni pamoja na kutulipa fidia ili waweze kuchukua maeneo hayo lakini sio
kutumia nguvu na vitisho kama inavyofanyika sasa.
Tumaini
letu ni kwako Rais Magufuli utakayeweza kutuokoa na janga hili ambalo
linasababisha tuishi kwa hofu huku tukishindwa kufanya shughuli zetu za
kila siku kwa kuhofu tukiondoka Dawasa wanawez kuingia na kubomoa makazi
yetu.
Pia
tunatambua kuwa wapo baadhi ya watendaji wamekuwa waking’ang’ania jambo
hilo kwa lengo la kutaka kutukosanisha na serikali yako nasi hatupo
tayari kuona jambo hilo likifanikiwa ndiyo maana tumelazimika kukibilia
kwako.
Tunakombea
Mungu akupe nguvu na afya tele ili uzidi kututetea sisi wananchi
wanyonge wa chini ambao tegemeo letu ni kwako Rais Magufuli.
Tunatanguliza shukrani zetu
Ni sisi wananchi wa Kata tano
Za jijini Dar Es Salaam.
No comments :
Post a Comment