WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amewataka wafanyabiashara wilayani Ruangwa kutumia taasisi za kifedha
kukopa fedha kwa ajili ya kukuza mitaji yao.
Ameyasema hayo leo (Jumapili,
Machi 25, 2018) wakati akizungumza na wafanyabiashara wa
wilaya hiyo
katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Chama Cha Walimu, wilayani
Ruangwa.
Waziri Mkuu ambaye yuko wilayani
Ruangwa kwa ziara ya kikazi ya siku mbili amesema ni vema wakatumia
taasisi za kifedha zilizopo ili kukuza mitaji yao.
”Naamini sekta ya biashara ni
muhimu katika mabadiliko ya maendeleo, hivyo wafanyabiashara ni chachu
ya maendeleo kokote na Serikali itaendelea kuwaunga mkono.”
Amesema katika kuhakikisha riba
zinapungua, Rais Dkt. John Magufuli anaendelea kuzungumza na wamiliki wa
taasisi za kifedha ili waone namna ya kupunguza riba hiyo.
Waziri Mkuu amesema lengo la
Serikali la kuchukua hatua hiyo ni katika kutekeleza mkakati wake wa
kuwawezesha wafanyabiashara ili waweze kupata mikopo yenye riba nafuu.
Pia Waziri Mkuu amewahakikishia
wananchi wa wilaya hiyo kwamba Serikali ipo pamoja nao na imedhamilia
kuboresha huduma mbalimbali za jamii kama maji na afya.
Naye, Mwenyekiti wa Umoja wa
Wafanyabiashara wa Wilaya ya Ruangwa, Bw. Said Shea amewaomba
wafanyabiashara wenzake watumie fursa za maendeleo zilizoko wilayani
humo kwa kupanua wigo wa biashara zao.
No comments :
Post a Comment