Waziri wa ulinzi wa Israel Mhe. Avigdor Liberman akimpa
zawadi mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa moyo nchini Israel alipotembelea
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo huku waziri wa afya, maendeleo
ya jamii, jinsia, wazee na
watoto Mhe. Ummy Mwalimu akishuhudia. Tangu mwaka 2015 JKCI kwa
kushirikiana na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart –
SACH) ya nchini Israel wanafanya kambi maalum za matibabu ya moyo kwa watoto.
Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Waziri wa ulinzi wa Israel Mhe. Avigdor Liberman wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto na wazazi wao ambao walifanyiwa upasuaji wa moyo nchini Israel. Mhe. Liberman alitembelea
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwa ajili ya kuona
ushirikiano ulipo kati ya JKCI na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a
Child’s Heart – SACH) ya nchini Israel ambao kwa kushirikiana wanafanya
kambi maalum za matibabu ya moyo kwa watoto ambapo watoto wanaokutwa na
matatizo yanayohitaji matibabu ya hali ya juu wanatibiwa nchini humo
bila malipo .
Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimpa zawadi ya kitenge Waziri wa ulinzi wa Israel Mhe. Avigdor Liberman alitembelea
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwa ajili ya kuona
ushirikiano ulipo kati ya JKCI na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a
Child’s Heart – SACH) ya nchini Israel ambao kwa kushirikiana wanafanya
kambi maalum za matibabu ya moyo kwa watoto ambapo watoto wanaokutwa na
matatizo yanayohitaji matibabu ya hali ya juu wanatibiwa nchini humo
bila malipo.
Waziri wa ulinzi wa Israel Mhe. Avigdor Liberman akisaini
kitabu cha wageni alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
leo kwa ajili ya kuona ushirikiano ulipo wa matibabu ya moyo kwa watoto,
kusomesha madaktari na wauguzi kati ya
JKCI na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya
nchini Israel. Kulia ni waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia,
wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Waziri wa ulinzi wa Israel Mhe. Avigdor Liberman wakiwa
katika picha ya pamoja na madaktari pamoja na wauguzi wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambao walisoma nchini Israel kwa udhamini wa
Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini
humo.
Picha na JKCI
No comments :
Post a Comment