WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa
amepongeza makubaliano yaliyofikiwa na nchi za Afrika za kulifanya bara
hilo kuwa eneo huru kibiashara.
Majaliwa aliyasema baada ya
kumaliza kusaini mkataba wa nchi za Afrika kuhusu mkataba huo
akimwakilisha Rais John Magufuli Jijini Kigali ambapo alisema Tanzania
imeajiandaa
vya kutosha kutekeleza mkataba huo.
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Kigali , Waziri Mkuu alisema Tanzania itahakikisha mkataba
huo unatelekezwa bila kuathiri huduma zinazozalishwa ndani.
Alisema Tanzania itahakikisha mikataba mitatu ambayo imesainiwa inatekelezwa bila kuathiri uzalishaji na sera za ndani.
Mikataba iliyosaioniwa na
mataifa hayo 50 ya Bara la Afrika ni pamoja na mkataba wa kulifanya bara
la Afrika kuwa eneo huru la biashara, Itifaki ya kisheria ya
utekelezaji wa makubaliano hayo ikiwamo uhuru wa makazi, haki ya kuishi
na kufanyakazi popote bila vikwazo wala vizuizi vyoyote.
Azimio la tatu ni Azimio la Kigali ambalo limejumuisha mawazo ya uanzishwaji wa mchakato huo.
“Nichukue fursa hii kumpongeza
Rais wa Rwanda na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Paul Kagame kwa
kutilia maanani suala hili hadi kufikia hatua hii ya kusaini mkataba.
“Tanzania kama wadau wakuu wa
mkataba huu tunakwenda kujipanga kuhakikisha mkataba huu unatekelezwa
bila kusababisha vikwazo vyovyote.
“Hata hivyo tunakwenda kupeleka
baadhi ya masuala haya katika vikao vya Baraza la mawaziri ili kuangalia
sheria zetu zisije kuwa kikwazo katika utekelezaji wa mkataba huu.
“Kwa mfano Tanzania tunayo sera
ya viwanda, lazima tuangalie ili tusije kuruhusu bidhaa kuingia nchini
mwetu na kuathiri biashara na bidhaa zetu za ndani.
Vile vile katika uhuru wa
biashara ya anga ambapo Tanzania bado tuna ndege chache ili tusije
kuruhusu kiholela, l;azima tuwe waangalifu katika hilo.
“Aidha Tanzania tumeruhusu maeneo
ya kuzalisha bidhaa, kwa hiyo lazima tuwe makini ili tusije kuruhusu na
kuharibu mwenendo wa kiuchumi.
Awali akihutubia katika ufunguzi
wa sherehe hizo, Rais wa Rwanda, Paul Kagame aliyataja maeneo makuu
ambayo mkataba huo umeangazia kuwa ni pamoja na eneo huru la biashara ya
anga, miundombinu ya reli na barabara ambayo itaziunganisha nchi za
Afrika kuwasiliana kwa urahisi.
Kagame ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Umoja wa Afrika (AU), alisema mkataba huo unatoa nafasi maalum ya
Ukanda wa Afrika kujali utu, kumnufaisha mkulima, mfanyabiashara na
wabia wengine wa maendeleo kuja kutafuta fursa Afrika.
“Azimio hili linatoa nafasi
kununu na kuuza bidhaa sambamba na kupata wabia duniani kote, biashara
huru itatuweka pamoja na muafaka wa Afrika tutakayo” alisema Rais
Kagame.
Mkataba huo ulisainiwa jana baada
ya vikao vya maadalizi vilivyohusisha timu za wataalam na mawaziri wa
biashara na mambo ya nje ya nchi zinazounda Umoja huo.
Tanzania ni miongoni mwa nchi 50 wanachama wa AU ambao walisaini mkataba huo.
No comments :
Post a Comment