Shirika
kubwa zaidi la kitanzania la mawasiano ya simu, na watoa huduma ya simu
zisizohamishika, broadband, bidhaa na huduma za internet wanaoongoza
Tanzania pamoja kampuni ya maisha ya kidigitali inayoongoza Tanzania,
Tigo. Leo wameingia katika ubia mkubwa, ambapo wateja kutoka katika
taasisi hizi mbili wataweza kutuma na kupokea fedha kati ya mitandao
hiyo miwili moja kwa moja katika akaunti zao.
Akiongea
wakati wa kutangaza ubia huo katika ukumbi wa Golden Jubilee Towers
Jijini Dar es salaam, Mkuu wa Idara ya Huduma za Fedha kwa njia ya simu
za mkononi wa TTCL, Moses Alphonce amesema kwamba, “Tunafuraha sana
kutia sahihi makubaliano ya ushirikiano huu ambao unaenda kuwanufaisha
wateja wetu na wananchi wote kwa ujumla. Ujio wa TTCL PESA katika sekta
hii ya mawasiliano ina lengo la kutengeneza ushirikishwaji wa
masuluhisho ya kifedha kwa watanzania wote. Lengo letu ni kubadilisha
mahitaji ya kila siku ya kifedha ya watu wetu yawe yasiyo ya fedha
tasilimu na kuwa wawezeshaji wa miamala yote ya kidigitali inayofanyika
Tanzania”.
Aliongezea
kuwa, tuna mifumo bora sana ambayo inaweza kutoa uwezo kwa makampuni na
taasisi za kiserikali uwezo wa kutoa malipo ya kidigitali kwa mamilioni
ya watanzania.
TTCL
PESA inatoa huduma ya kifedha ya kidigitali ambayo ni bei nafuu, ya
haraka na salama ambayo inazidi huduma za benki kupitia simu za mkononi,
huduma za malipo, kuongeza muda wa maongezi na uhamishaji wa fedha.
Kwa
upande wake, Afisa mkuu wa Huduma za kifedha za simu za mkononi wa
Tigo, Hussein Sayed amesema kwamba makubaliano haya kuwa ni mwanzo wa
ushirikiano mkubwa lakini pia jukumu la uanzilishi la Tigo katika huduma
za fedha kupitia simu za mkononi, ushirikiano tayari umeshasainiwa.
Jambo hili limeziakikishia kampuni hizi mbili zenye shauku ya kuwapatia
wateja wao huduma ya kiwango cha juu katika zama hizi za huduma za
kifedha za kidigitali. “Kwa makubaliano haya kwa mara nyingine tena
tunaisaidia Tanzania kuimarisha jukumu lake lisiliokwepeka katika
waanzailishi wa ushirikishwaji wa kifedha kwa njia za kidigitali
duniani. Ushirikiano mara zote huwa ni chachu ya ukuaji katika sekta ya
fedha kwa njia za simu za mkononi.” Alisema Sayed.
“Tumetambulisha
sokoni idadi kadhaa ya bidhaa zenye ubunifu na tuna nia ya kupanua
watumiaji wetu kwa kushirikiana na watoa huduma wenzetu walioko sokoni”
Aliongeza Hussein.
Katika
mwezi June 2014, Tigo iliibuka kuwa ya kwanza baada ya kufanikiwa
kuzindua makubaliano ya ushirikiano ya kwanza ya aina yake ambayo
yanawawezesha mamilioni ya wateja wa Tigo Pesa kutuma fedha na kupokea
fedha kwa watoa huduma wengine waliosajiliwa.

No comments :
Post a Comment