Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Innocent
Bashungwa akisisitiza jambo kwa watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais
(hawapo pichani) mara baada ya kupokea taarifa ya Ofisi ya Makamu wa
Rais na kujadili utelekezaji wa Bajeti ya Ofisi hiyo kwa mwaka fedha
2017/2018 na mapendekezo ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2018/19.
Taarifa iliyowasilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba. Kulia ni Katibu wa Kamati
Bw. Wilfred Magova.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira)Mhe. January Makamba, Naibu Waziri Mhe.
Kangi Lugola na Katibu Mkuu Mhandisi Joseph Malongo wakifuatilia
majadiliano ya wajumbe wa kamati mara baada ya kuwasilisha taarifa yao
kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, hii leo
Mjini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Kangi Lugola, Katibu Mkuu Mhandisi
Joseph Malongo na Naibu Katibu Mkuu Bi. Butamo Phillip wakifuatilia
majadiliano ya wajumbe wa kamati mara baada ya kuwasilisha taarifa yao
kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda Biashara na Mazingira, hii leo
Mjini Dodoma.
Pichani wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Viwanda Biashara na Mazingira Mhe. Hawa Subira
Mwaifunga na Mhe. Omary Ahmed Badwel wakifuatilia majadiliano katika
Kamati yao hii leo Mjini Dodoma.
Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Viwanda Biashara na Mazingira Mhe. Kanali (Mst)
Masoud Ali Khamis na Mhe. Zainab Mdolwa Amiri wakifuatilia majadiliano
kikaoni hapo.
………………….
YALIYOJIRI KWA UFUPI WAKATI WAKUWASILISHA TAARIFA KATIKA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA 22/03/2018
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba
#Kwa kiasi kikubwa kiwango cha
uelewa kwa wananchi na jamii kwa ujumla juu ya masuala ya mazingira
kimeongezeka na Ofisi ya Makamu wa Rais itaendelea kutoa elimu kwa Umma
na suala hili litapewa kipaumbele
#Ofisi ya Makamu wa Rais inashirikiana na wadau mbalimbali katika kuhamasisha uwekezaji endelevu na rafiki kwa mazingira.
#Matumizi ya nishati mmbada wa
mkaa yanaendea kuhimizwa ikiwa ni pamoja na matumizi ya gesi na matumizi
ya majiko banifu na matumizi ya tungamotaka (Bio-Mass).
#Zaidi ya Maafisa Mazingira mia
tano (500) wameteuliwa kwa ajili ya kuwa ’wakaguzi wa
Mazingira’ambao
watafanya kazi kwa mujibu wa sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004 kifungu
namba 182 (2)
#Serikali inaendelea kujenga uwezo wa Taasisi ikiwemo NEMC ili iweze kutimiza majukumu yake ipasavyo kwa mujibu wa Sheria.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Kangi Lugola
#Serikali imeanzisha Mfuko wa
Mazingira ambao pamoja na mambo mengine fedha yake itasaidia kampeni
kubwa ya upandaji miti hapa nchini
#Taasisi/Vikundi vinavyojihusisha
na masuala ya hifadhi na usimamizi wa mazingira nchini vinaweza kupewa
tuzo ili kutoa chachu kwa vikundi vingine pia
#Kila Wilaya na Halmashauri
zinatakiwa kuanzisha Sheria ndogo ndogo kwa ajili ya Hifadhi na
usimamizi wa Mazingira katika maeneo yao.
#Serikali imeanza mchakato wa
kuandaa orodha ya wachimbaji wadogo wadogo wote hapa nchini ili
uandaliwe utaratibu maalumu wa kuwaratibu kwa ujumla wao.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Innocent Bashungwa
#Kampeni za kitaifa za Mazingira zinaonekana na vema juhudi hizi ziendelee kwa kushirikisha wadau wote
#Serikali iangalie upya matumizi
ya Mkaa wa kuja na nishati mbadala ili kunusuru ukataji wa miti
unaoendelea kwa kasi, ikiwa ni pamoja na kushirikiana na SIDO katika
kutengeneza majiko banifu
#Usimamizi wa Sheria ya Mazingira
uzingatiwe ikiwa ni pamoja na kuitaka Migodi mikubwa kufuata taka la
kisheria la kurudhisha hali ya mazingira ya awali mara baada ya
kukamilika kwa uchimbaji.
No comments :
Post a Comment