Katibu wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA) Merinah Millensasha (kulia) akionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) cheti cha pongezi kwa kazi ya uzalendo inayofanywa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk Hassan Abbasi (katikati) na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto wa asasi hiyo, Mohamed Shaban.
Katibu wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA) Merinah Millensasha (kulia) akimkabidhi cheti cha pongezi Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk Hassan Abbasi (katikati) kwa kutambua kazi ya Uzalendo anayofanya, kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto wa asasi hiyo, Mohamed Shaban.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk Hassan Abbasi (katikati) akionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) cheti cha pongezi kwa Uzalendo alichokabidhiwa na Katibu wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA) Merinah Millensasha (kulia) na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto wa asasi hiyo, Mohamed Shaban.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbasi (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhiwa cheti cha pongezi kwa kazi ya Uzalendo anayofanya na Katibu wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA) Merinah Millensasha (kulia) na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto wa asasi hiyo, Mohamed Shaban.
Cheti cha pongezi alichokabidhiwa
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk
Hassan Abbasi kwa kutambua kazi ya uzalendo anayoifanya.
Picha na Idara ya Habari – MAELEZO
…………….
Na Jonas Kamaleki- MAELEZO
Asasi ya Wazalendo na Maendeleo
Tanzania (AWAMATA ) imempatia tuzo Mkurugenzi wa Idara ya Habari (
MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi kwa kazi zake
za kizalendo anazozifanya kwa niaba ya wananchi.
Tuzo hiyo ambayo ni cheti
ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu wa AWAMATA, Mkoa wa Dar es
Salaam, Merinah Millensasha ambaye aliongozana na kiongozi mwingine wa
asasi
hiyo, Muhammad Shaban Aluta.
“Dkt. Abbasi ni Mzalendo wa kweli
kutokana na kazi anazozifanya kwa ajili maendeleo ya Taifa, hivyo
tumeona nai vyema kumpatia cheti tukitambua mchango wake katika jamii”,
alisema Millensasha.
Alisema kuwa Dkt. Abbasi amekuwa
mbunifu wa mambo mengi ikiwemo kipindi cha TUNATEKELEZA na jarida ambalo
linafafanua mambo mengi yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano.
Akitoa shukrani kwa tuzo hiyo,
Dkt. Abbasi amesema kuwa nashukuru kwa tuzo hiyo ambayo imetolewa na
watu ambao hakuwafahamu kabla pia ni tuzo ya kwanza kuipata tangu
alivyokabidhiwa madaraka hayo miezi kadhaaa iliyopita.
“Tunaendela kutekeleza kwa kasi
majukumu ya Taifa ili kuhakikisha nchi yetu inapiga hatua kubwa
kimaendeleo”, alisema Dkt. Abbasi.
Aliongeza kuwa Tanzania imedhamiria kuwavusha watanzania na haitarudi nyuma katika suala la kuwaletea maendeleo wananchi.
Aidha, Dkt. Abbasi amesema ni
dhahiri kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inafanyakazi kwa vitendo.
Imeanzana vita dhidi ya rushwa na ufisadi, inajenga miundombinu ya reli,
barabara za chini na za juu na kuweka miundombinu ya uhakika ya
kuzalisha umeme.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo,
yote haya ni kuonyesha kuwa Tanzania ya sasa inalenga katika kuboresha
hali za wananchi na hasa wa kipato cha chini.
AWAMATA ni asasi isiyo ya kiserikali inayofanya shughili ya kuhamasisha uzalendo ambao unaonekana kupotea kwa walio wengi.
No comments :
Post a Comment