Simu ya Smartphone yenye GB 3 za internet bure kila mwezi kwa muda wa miezi sita kutoka Tigo.
Tarehe 22 Machi 2018, Dar es Salaam.
Wapenzi
wa smatphone wanayo sababu nyingine ya kutabasamu baada ya kampuni
inayoongoza ya mtindo wa maisha ya kidigitali, Tigo Tanzania kuungana na
kampuni ya Samsung Electronics Tanzania kwaajili ya kuwapatia wateja
wake nafasi ya kwanza kumiliki simu mpya ya kisasa ya Sumsang S9 na
Samsung S9+ zilizojazwa bando la bure la internet ya 3 GB kila mwezi kwa
miezi sita kutoka Tigo.
‘Tigo
ni kampuni pekee ya simu za mkononi na ya kwanza kuwa na simu mpya za
kisasa za Samsung S9/S9+ nchini. Hakuna mwendeshaji mwingine yeyote wa
mtandao wa simu au duka ambalo tayari limeshapokea simu hizi za kisasa
za smartphone,’ Mkuu wa idara ya Bidhaa na Hudumawa Tigo (Head of Products and Services), Davidi Umoh aliabainisha.
Umoh
aliongeza kuwa ‘Tigo imeshika usukani wa mabadiliko ya mtindo wa maisha
ya kidigitali . Tuna lenga katika kuendelea kuongeza upatikanaji wa
simu za smartphone nchini wakati huo huo tukiwa tunahakikisha kuwa
wateja wetu wote wanafurahia huduma bora za kidigitali kupitia mtandao
wetu wenye kasi zaidi wa 4G ambao ndio uliosambaa zaidi hapa nchini.
Akielezea kuhusu Ushirikiano uliopo, Meneja wa Samsung Electronics nchini Tanzania, Suleiman Mohammed amesema”Tunajisikia fahari sana kushirikiana na Tigo kwaajili ya kuleta fursa za kusisimua na ofa kwa wateja wa Tanzania. Hii ni hatua ya msingi sana katika ukuzaji wa sekta ya simu za mkononi ambayo inaruhusu wateja kupata simu za kisasa katika wakati huo huo ambapo simu hizo zinazinduliwa duniani kote”.
Kuna
njia tatu za kununua simu ya smartphone ya Samsung S9/S9+ Kwanza mteja
anaweza kutembelea duka lolote la Tigo nchi nzima nakulipia na kujipatia
simu mpya ya kisasa aina ya Samsung S9 na S9+. Njia ya pili ya kununua
simu hizo nikutembelea Tigo Store katika ukurasa wa mtandao wa manunuzi
wa jumia www.jumia.co.tz/tigo-shop.
Mwisho wateja wanaweza kupiga menyu mpya ya Tigo *147*00# na kisha
kuchagua duka la simu ambako utaweza kuchagua namna ya kulipia ambayo
inaruhusu kulipia kidogo kidogo na kuchukua simu yake baadae.
Simu
za smartphone za kisasa za Samsung S9/S9+ zinapatikana katika rangi
nyeusi, kijivu na zambarau na zitauzwa reja reja kwa bei ya TZS
2,049,000 kwa Samsung S9 na TZS 2,315,000 kwa Samsung S9+.
No comments :
Post a Comment