Na Mahmoud Ahmad Arusha
Wachimbaji
wadogo wameendelea kusotea eneo lao kwa mikataba migumu inayowagawa na
kuwafukuza katika maeneo yao ambapo kumekuwapo na utambulisho wa leseni
tofauti tofauti katika eneo moja na kuwaacha na sintofahamu na kuelekeza
lawama kwenye ofisi za Kamishna msaidizi kanda ya kati Sosthenes Masola
kwa kuendelea kubariki leseni kwa kummilikisha mtu mmoja huku akitambua
ana maombi halali ya wachimbaji wadogo kwenye ofisi yake bila majibu
hadi sasa wakati sheria ya madini ya mwaka 2010 inasema ni ndani ya siku
28 majiubu yanakuwa teyari huku Coordness zikiksoma maombi ya
wachimbaji ndani ya wizara ya madini.
Leseni
hizo ambazo zimekuwa zikitolewa baada ya mh. raisi kuzuiya utoaji wa
leseni hadi itakapoundwa tume zinaonekana kutaka kuwakimbiza wachimbaji
katika eneo hilo kwa kigezo cha umiliki wa leseni jambo ambalo
wanaziomba mamlaka kulitupia macho jambo hilo kwa uwepo wa hadaa na
ukwepaji wa kodi za serikali kama ilivyobainishwa katika kikao cha
mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Fallesy Kibassa na wachimbaji terehe
1\12\2017 kata ya Changaa.
Akizungumza
kwa niaba ya wachimbaji hao Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo Juma
Ramadhani Chuha amesema kuwa lengo la muongozo wa mkuu wa wilaya ya
Kondoa bi Sezaria Makota kumaliza mgogoro linaonekana kugonga mwamba kwa
hatua hii ya kuingia mikataba ya maduara badala ya kikundi kwa mkutano
halali wa kisheria ambao ulitolewa muongozo.
Amesema
badala yake amekuwa akiwaita wachimbaji kinyemela na kuwapa mikataba
badala ya kukaa nao na kujadili namna nzuri ya kuainisha haki za
wachimbaji na uwepo wao katika eneo lao la mgodi badala yake kumekuwepo
na taratibu za kuwaondoa katika maeneo yao kwa mikataba batili ya
vichochoroni badala ya kuitisha mkutano huru wa wachimbaji wote.
“kwa
mujibu wa muongozo wa kamati ya ulinzi na usalama kuwataka pande zote
kushirikiana na mwanasheria wa halmashauri ili kupata ufafanuzi wa
kisheria jambo hilo limekiukwa na kuwa kitendawili cha kutoheshimu
sheria na maamuzi ya vikao” alisisitiza Chuha
Nae
Moja wa wachimbaji wadogo wa madini kwenye kijiji cha BubuChangaa
Mataka Iddy alisema kuwa lengo lao lilikuwa ni kufikia kumiliki eneo
hilo kisheria na kulipa mapato ya serikali lakini cha kushangaza mamlaka
zinatutaka tuwe chini ya mmiliki wa leseni batili ambazo ni no 005012CZ
na 005013CZ ambaye wakati tunaomba eneo hilo hakuwepo wala maombi yake
yalitumwa nyuma ya maombi yetu na kupimiwa eneo na kulipia cha
kushangaza sisi hatujapewa majibu hadi sasa kama tulikosa au kupata .
Amesema
kuwa kimsingi wataendelea kudai haki zao hata kwa kufika kwa mh.Rais
kwani wamekuwepo kisheria na wanaendelea kusotea kusimamishwa kazi kwa
migogoro ilioanzishwa na wachimbaji wenzao kwa kushirikiana na mporaji
wa maeneo kwa leseni mpya no 006092CZ hadi 006099CZ ambazo hapo awali
kwenye kikao cha mgogoro hazikutambulishwa kwani wilaya yote imekuwa ni
mali yake kwasasa katika migodi na anamiliki leseni zaidi ya 20 zisizo
na tija wala ajira kwa vijana wa changaa na wilaya kwa ujumla.
Amesema
kuwa pamoja na mamlaka mbali mbali walizoziendea kushindwa kutambua
uhalali wa maombi yao kimsingi na majibu ya Afisa madini mkazi Kondoa
Silimu Tegalile kusema wazi kuwa anamiliki leseni mbili inaonekana kuwa
ni kinyume na alivyoainisha mbele ya mkuuu wa wilaya bi Sezaria Makota,
jambi hili inaonekana kukidhana na leseni zinazotambulishwa kwa sasa
kwenye mkataba aliotupatia wachimbaji, kwani wali zozitambulisha mbele
ya mkuu wa wilaya ni leseni mbili kwenye mkataba zipo saba.



No comments :
Post a Comment