Na Emmanuel J. Shilatu
1. Anatutoa kwenye
usafiri wa treni wa enzi za kikoloni unaotumia muda mrefu njiani
anatupeleka kwenye usafiri wa treni wa kisasa unaotumia umeme na muda
mchache njiani kusafirisha Watu wengi na mizigo mingi.
2. Anatutoa kwenye usafiri wa anga wa ndege uliokufa anatupeleka kwenye ufufuo wa shirika la ndege lenye ndege mpya sita.
3. Ametutoa kwenye
shirika la simu lililokufa ametupeleka kwenye ufufuo wa shirika la simu
linaloleta ushindani mkubwa kwenye makampuni ya simu yaliyokuwapo
kutokana na ubora wa huduma na wa gharama nafuu.
4. Ametutoa kwenye uchumi uliokuwa asilimia 5.1 mwaka 2015 mpaka kutupeleka kwenye uchumi unaokuwa wa zaidi ya asilimia 7.2
5. Ametutoa kwenye mzigo wa kulipia elimu mpaka kutupeleka kwenye unafuu wa elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari.
6. Amewatoa akina Mama
Wajawazito kwenye mateso ya kujifungulia sakafuni ametupeleka kwenye
faraja kwa akina Mama Wajawazito kujifungulia vitandani. Mjamzito mmoja,
kitanda kimoja.
7. Ametutoa kwenye
mateso ya kulanguliwa dawa na ukosefu wa dawa kwenye hospitali za
Serikali ametupeleka kwenye upatikanaji wa madawa mahospitalini
uliofikia kiwango cha upatikanaji cha asilimia 89, tena kwa bei nafuu.
8. Ametutoa kwenye
usumbufu na mateso kwa Wamachinga na Mama Ntilie kusumbuliwa na Wagambo
mpaka kutupeleka kwenye utulivu na amani ya kutosumbuliwa kwa Wamachinga
na Mama Ntilie.
9. Ametutoa kwenye mfumo
wa kuleana na kuchekeana dhidi ya wabadhilifu na wala rushwa na
kutupeleka kwenye mfumo wa uwajibikaji wa kupelekwa mahakamani kwa wala
rushwa na Mafisadi. Leo hii Tanzania imepanda kwa nafasi kwa nafasi 13
katika mwaka 2016 na mwaka 2017 na pia ikishika nafasi ya pili kwa nchi
za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
10. Ametutoa kwenye
mateso ya Wanafunzi kukaa chini kwa kukosa madawati na kukosa maabara.
Leo hii ametupeleka kwenye hatua ya ukamilifu wa uondoshaji wa tatizo la
madawati nchi nzima na maabara kwa baadhi ya shule.
11. Anatutoa kwenye
uondoshaji wa tatizo la foleni jijini Dar na kutupeleka kwenye ujenzi wa
barabara za juu (flyovers) za Tazara na Ubungo.
12. Amewatoa Wanazuoni
wa chuo kikuu cha UDSM kwenye mateso ya kupanga na leo hii amewapeleka
kwenye makazi bora ya mabweni ya kisasa wanayolipia gharama za chini
kabisa.
13. Ametutoa kwenye
balaa la utendaji na uwajibikaji wa hovyo kwa Watumishi wa umma na
ametupeleka kwenye uimarishwaji wa kiwango cha kuridhisha cha
uwajibikaji na uadilifu kwa Watumishi wa umma.
14. Ametutoa kwenye
utitiri wa kodi kwenye kilimo na kutupeleka kwenye ufutwaji wa kodi
mbalimbali za kilimo na kukifanya kuwa chenye tija kwa Wakulima. Leo hii
bei ya korosho imepanda kutoka Tsh. 800 kwa kilo mpaka kufikia Tsh.
4000 kwa kilo.
15. Ametutoa kwenye
usiri mkubwa wa mikataba na taarifa za madini na kutupeleka kwenye uwazi
taarifa na mikataba ya madini. Leo hii tunajivunia mafanikio ya gawio
sawia la faida za madini na Serikali ikimiliki asilimia 16 ya hisa
katika makampuni ya uchimbaji wa madini.
16. Ametutoa kwenye
tatizo zito na sugu la ajira na kutupeleka kwenye ongezeko la fursa za
ajira kupitia kwenye viwanda zaidi ya 3000, kuwatimua wenye vyeti vyeki,
miradi ya ujenzi ya bomba la mafuta, flyovers na reli ya kisasa ya
standard gauge.
17. Ametutoa kwenye
makusanyo ya Tsh. Bilioni 800 kwa mwezi mpaka kufikia kwenye makusanyo
ya Tsh. Trilioni 1.5 kwa mwezi. Hali hiyo imeimarisha uwezo wa Serikali
kibajeti.
18. Ametutoa kwenye
urasimu na umangimeza kwa viongozi na kutupeleka kwenye uimarishwaji wa
kiwango cha nidhamu, uwajibikaji na uadilifu kwa viongozi wa Serikali.
Leo hii hakuna usumbufu kumuona kiongozi na viongozi wengi wapo site
palipo shida za Wananchi wakizitatua.
19. Ametutoa kwenye
mfumo wa walio nacho kujiona Mungu mtu na kuleta ukandamizi ndani ya
jamii na kutupelekea kwenye uondoaji wa tabaka la uonevu kwenye masuala
ya ardhi na sheria.
20. Ametutoa kwenye
mkwamo wa Serikali kuhama Dar es Salaam na kutupeleka kwenye hamisho la
Serikali kuhamia Dodoma. Mpaka sasa Waziri Mkuu, Wizara na idara
mbalimbali zimehamia Dodoma. Tukumbuke mpango wa Serikali kuhamia Dodoma
ulikuwepo na kushindikana kufanyika toka enzi za utawala wa Serikali ya
awamu ya kwanza.
No comments :
Post a Comment