Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Amina
Masenza (katikati) akizungumza na waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (kulia) alipofanya ziara katika mkoa wa
Iringa kukagua maeneo yaliyotumika kama kambi za wanaharakati wa Urithi
wa Ukombozi wa Bara la Afrika jana Mkoani Iringa. Kushoto ni Katibu
Tawala Mkoa wa Iringa Bibi. Wamoja Ayubu
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (kulia) akifafanua jambo wakati wa
ziara yake katika mkoa wa Iringa kukagua maeneo yaliyotumika kama kambi
za wanaharakati wa Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika jana Mkoani
Iringa. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Amina Masenza na kushoto
ni Katibu Tawala Mkoa wa Iringa Bibi. Wamoja Ayubu
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (kushoto) akisalimiana na askari
magereza wa gereza la Mgagao lililopo katika wilaya ya Kilolo mkoani
Iringa alipotembelea gereza hilo jana kama moja ya kambi iliyotumiwa na
wapigania uhuru kutoka Afrika ya Kusini wakati wa ziara yake katika mkoa
wa Iringa kukagua maeneo yaliyotumika kama kambi za wanaharakati wa
Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya
Kilolo Mhe. Asia Abdala
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza
nyimbo za kihehe wakati wa ziara ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe katika mkoa wa Iringa kukagua maeneo
yaliyotumika kama kambi za wanaharakati wa Urithi wa Ukombozi wa Bara la
Afrika jana Mkoani Iringa.
Vijana walio na mchanganyiko wa
kitanzania na Kizulu wakiimba wimbo wa taifa wa Afrika ya Kusini wakati
wa ziara ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison
Mwakyembe katika mkoa wa Iringa kukagua maeneo yaliyotumika kama kambi
za wanaharakati wa Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika jana Mkoani
Iringa.
Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe. Asia
Abdala (aliyesimama) akizungumza na wananchi wa wilaya ya Kilolo wakati
wa ziara ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison
Mwakyembe (kulia) katika mkoa wa Iringa kukagua maeneo yaliyotumika kama
kambi za wanaharakati wa Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika jana
Mkoani Iringa.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (aliyesimama) akizungumza na wananchi
wa Lugalo alipotembelea mnara wa Lugalo walipozikwa Askari 300 wa
kijerumani pamoja na kiongozi wao wakati wa ziara yake katika mkoa wa
Iringa kukagua maeneo yaliyotumika kama kambi za wanaharakati wa Urithi
wa Ukombozi wa Bara la Afrika jana Mkoani Iringa. Kushoto ni Mkuu wa
Wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Abdala
Baadhi wa wananchi wa Kilolo
wakimsikiliza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison
Mwakyembe (hayupo pichani) wakati wa ziara yake katika mkoa wa Iringa
kukagua maeneo yaliyotumika kama kambi za wanaharakati wa Urithi wa
Ukombozi wa Bara la Afrika jana Mkoani Iringa.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (aliyeshika mkuki) katika picha ya
pamoja na wananchi wa Lugalo alipotembelea Mnara wa Lugalo walipozikwa
Askari 300 wa kijerumani pamoja na kiongozi wao wakati wa ziara yake
katika mkoa wa Iringa kukagua maeneo yaliyotumika kama kambi za
wanaharakati wa Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika jana Mkoani Iringa.
Kushoto kwa waziri ni Mkuu wa Wilaya ya
Kilolo Mhe. Asia Abdala
Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM
………………….
Na: Genofeva Matemu – WHUSM
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezi Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka viongozi wa Mkoa wa
Iringa kuhamasisha wananchi wa Iringa kutunza utalii na historia ya
ukombozi wa Bara la Afrika kwa kuthamini nafasi iliyopewa nchi ya
Tanzania kuwa mwenyeji wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la
Afrika.
Waziri Mwakyembe ameyasema hayo
jana Mkoani Iringa alipofanya ziara katika mkoa huo kukagua maeneo
yaliyotumiwa na wapigania uhuru wa kusini mwa Afrika na kusema kuwa
kihistoria Tanzania imepewa heshima kubwa na Umoja wa Afrika kutokana
na mchango mkubwa iliyotoa wakati wa harakati za ukombozi wa Bara la
Afrika.
“Zoezi la kuhifadhi nyaraka za
kumbukumbu ya ukombozi wa bara la Afrika ni letu sote, linatusaidia
waafrika kuandika upya historia yetu kutokana na kasi ya maendeleo ya
kiteknolojia hivyo wajibu wetu sote kuwaandaa vijana ili wawe na uwezo
wakuwezesha na kurithisha historia ya urithi wa ukombozi kwa vizazi
vijavyo ndani na nje ya nchi” amesema Mhe. Mwakyembe
Aidha Mhe. Mwakyembe amesema kuwa
Mnara wa Lugalo walipozikwa askari wa kijerumani 300 na kiongozi wao ni
moja ya ishara ya ushujaa na uzalendo ulioonyesha uimara wa watanzania
kipindi cha harakati za ukombozi wa Bara la Afrika na kuahidi kuwa
serikali itayalinda, kuyatunza na kuyaendeleza maeneo yote yaliyotumika
katika harakati hizo ili vizazii vya Afrika vipate fursa ya kujua
historia tuliyopitia wakati wa kujikomboa.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Iringa Mhe. Amina Masenza ametoa wito kwa watanzania wote walio na
habari za kihistoria kujitokeza na kuweza kutoa historia hiyo ili waweze
kutenda na kutimiza wajibu woa kwa manufaa ya watanzania wote na
kuijenga na kuisimamisha Tanzania kihistoria kwani historia ni jambo hai
lisilokufa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe.
Asia Abdala amesema kuwa wilaya yake chini ya serikali ya awamu ya tano
itahakikisha kuwa inarejesha misingi ya utamaduni wa mtanzania na
historia nzuri iliyojengwa katika Bara la Afrika kwani Iringa inasifika
kwa historia hiyo na kama kwa pamoja serikali kwa kushirikiana na
wanairinga watayaendeleza maeneo yaliyotumika katika harakati za
ukombozi utalii na uchumi wa mkoa wa Iringa vitakua.
No comments :
Post a Comment