Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti, wakiangalia bia inavyopikwa katika kiwanda cha bia TBL tawi la Mwanza, walipotembelea jijini huo jana.
Wajumbe wa kamati ya Bunge wakitembea maeneo mbalimbali ya kiwanda
Mkurugenzi wa kiwanda cha Konyagi(TDL|) Devis Deogratius akiwasilisha mada ya utendaji wa kampuni ya bia TBL kwa Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti, walipotembelea kiwanda cha jijini Mwanza
Meneja wa kiwanda cha bia TBL tawi la Mwanza Marietha Mazula, akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti, walipotembelea kiwanda hicho jijini Mwanza
……………….
Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti mwishoni mwa wiki ilitembelea kiwanda cha
kutengeneza Bia cha TBL cha Mwanza kilichopo chini ya kampuni ya TBL
Group ambapo waliweza kutembelea vitengo mbalimbali vya uzalishaji sambamba na kupata maelezo jinsi kiwanda kinavyoendeshwa.
Meneja wa TBL Mwanza,Marietha Mazula,aliwaeleza wajumbe wa kamati hiyo mikakati mbalimbali ambayo inafanywa na kampuni ya TBL Group kuhakikisha inaimarika zaidi katika kufanikisha kwa vitendo mkakati wa serikali ya awamu ya tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
Baadhi
ya mikakati ambayo kampuni imeanza kutekeleza aliitaja kuwa ni kuwekeza
katika kutumia teknolojia za kisasa katika uzalishaji sambamba na
kuwezesha wakulima wanaoiuzia kampuni malighafi ili kuhakikisha kukua
kwa viwanda kunakuza sekta ya kilimo pia na kupunguza tatizo la ajira
nchini.
No comments :
Post a Comment