Judith Ferdinand, BMG
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,
John Mongella amewataka Wenyeviti wa Halmashauri na viongozi mbalimbali
wa mkoa kuweka utaratibu wa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhumi wa
bima ya afya.
Aliyasema hayo jana
kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC) kilichohudhuliwa a
viongozi mbalimbali wa Serikali ,dini na wanasiasa, alisema ni vema
kuhakikisha wananchi wanapatiwa elimu ili waweze kutambua umuhimu
wa kutumia bima ya afya.
Mongella alisema
anasikitika kuona watu hawatambui muhimu wa kujiunga na bima ya afya
kwani hurahisisha matibabu na gharama yake ni ndogo tofauti na mtu
ambaye hatumii huduma hiyo.
Alisema ili kuweza
kupunguza vifo kwa wananchi ni vema kila kiongozi kuweka utaratibu wa
kuelimisha jamii katika maeneo yao lengo ikiwa kupunguza na kumaliza
tatizo hilo kwani watapata matibabu wakati wote.
“Ili tuweze kupunguza
vifo vya watoto na wananchi kwa ujumla ni vema kuweka utaratibu wa
kuwaelimisha wananchi kuhusu kutumia bima ya afya kwani inasaidai pindi
ukiwa hauna hela na unaumwa au kuuguliwa,”alisema Mongella.
Pia alisema, ni dhambi
kutoa hamasisha wananchi kuhusu kutambua faida ya bima ya afya ambayo
ni mkombozi kwa wenye hali ya chini kwani hutumia pesa nyingi katika
matibabu wakati viongozi wanatumia na wamejiunga huduma hiyo.
Naye Clement Pancras
Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Part (DP) alisema ni vema kwa
viongozi kuhamasisha wananchi katika mambo ya msingi ikiwemo bima ya
afya kwa ustawi wa maisha yao na taifa kwa ujumla.
Alisema kila mwanachi
atakapokuwa na bima itasaidia hasa wenye hali ya chini ingawa changamoto
iliyopo ni hupatikanaji wa dawa ambao itamlazimu mgonjwa kutoa fedha za
kununulia, hivyo aliiomba serikali kupeleka na kuhakikisha dawa zote
zinapatikana katika hospitali zote na kuleta maana halisi ya kutumia
huduma hiyo.
No comments :
Post a Comment