Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi ,Mhandisi Hamad Masauni, akiwasili katika Viwanja vya Polisi
Oysterbay wakati wa Uzinduzi wa Vituo vya Polisi Vinavyohamishika lengo
ikiwa ni kusogeza huduma za kipolisi karibu na wananchi.Kulia ni Kamanda
wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa na wengine
kutoka kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Salum
Hamduni, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, Emmanuel Lukula na
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Jumanne Muliro.Tukio hilo
limefanyika mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, akimuongoza Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, kukagua mazingira ya ndani ya moja
kati ya Vituo vya Polisi Vinavyohamishika baada ya kuzinduliwa mwishoni
mwa wiki na naibu waziri huyo lengo ikiwa ni kusogeza huduma za
kipolisi karibu na wananchi.Uzinduzi huo ulifanyika katika Viwanja vya
Polisi Oysterbay,jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Polisi
Jamii Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Ahmada Khamis(kulia), baada ya
kuzindua Vituo vya Polisi Vinavyohamishika katika Viwanja vya Polisi
Oysterbay, lengo ikiwa ni usogezaji karibu wa huduma za kipolisi kwa
wananchi.Katikati ni Mkuu wa Shirika linaloshughulika na Usafirishaji
wa Wakimbizi nchini (IOM), Dk. Qasim Sufi.Tukio hilo limefanyika
mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akijibu maswali ya Waandishi wa Habari
baada ya Uzinduzi wa Vituo vya Polisi Vinavyohamishika lengo ikiwa ni
usogezaji wa huduma za kipolisi kwa wananchi.Tukio hilo limefanyika
mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Polisi Oysterbay, jijini Dar es
Salaam
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wanne kulia), akiwa katika picha ya pamoja
na viongozi mbalimbali wa Jeshi la Polisi na wageni waalikwa baada ya
kuzindua Vituo vya Polisi Vinavyohamishika, lengo ikiwa ni kusogeza
huduma za kipolisi kwa wananchi. Waliosimama ni Kikundi cha Polisi Jamii
cha Mkoa wa Kipolisi Kinondoni.Tukio hilo limefanyika mwishoni mwa wiki
katika Viwanja vya Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments :
Post a Comment