Kuelekea Maadhimisho ya
Siku ya Wanawake Duniani, Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, tunapenda kuwafahamisha wanawake, jamii na wadau
wengine kuwa Maadhimisho ya Mwaka huu yatafanyika katika ngazi ya Mikoa.
Kaulimbiu ni “Kuelekea Uchumi wa
Viwanda: Tuimarishe Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji Wanawake Vijijini”.
Kupitia kaulimbiu hii wadau wote tunaaswa kuongeza kasi ya kuwezesha
kufikiwa kwa usawa wa jinsia na kuwawezesha wanawake wa vijijini
kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni ili waweze kunufaika na fursa
mbalimbali katika kuelekea uchumi wa kati na wa viwanda.
No comments :
Post a Comment