Dar es Salaam, Marchi 2, 2018 –
‘Wateja 84 wa Tigo wiki hii wamejishindia simu za Smartphone aina ya
TECNO R6. Hii ni Droo ya nne ya Promosheni inayoendelea ya Tigo NYAKA
NYAKA inayowawezesha wateja wa Tigo kujishindia simu mpya za kisasa
zenye uwezo wa 4G na jumla ya simu 12 utolewa kwa kila siku.
Akizungumza
na waandishi wa habari Meneja wa Biashara wa Tigo, Suleiman Bushagama
alisema “Hii ni sehemu ya kuwawezesha wateja wetu waweze kutumia simu za
kisasa zenye uwezo wa 4G ili wafuruhie kuperuzi intaneti na kuweza
kuangalia mambo mbalimbali kwenye simu zao”.
Aliongeza
“Wateja wa Tigo Tanzania wanazidi kupata faida lukuki ikiwemo bonasi za
hadi GB 1 bure kwa matumizi yao ya intaneti pamoja na fursa ya kushinda
mojawapo ya simu janja 800 ambazo bado zinashindaniwa katika Nyaka
Nyaka Bonus, promosheni murua inayowazawadia wateja wa Tigo wanaounua
vifushi vya kuanzia TZS 1,000 vya intaneti kupitia menu iliyoboreshwa ya
*147*00# “.
Kwa
upande wa washindi mzee Issa Salum mkaazi wa Mbagala alisema “Sikuwa
naamini mara baada ya kupigiwa simu nilijua matapeli wa mjini wenye
kurubuni watu, baadae nikaamini nilipopewa maelezo yaliyojitosheleza”
Naomba niseme hivi Tigo sio wababaishaji ni ukweli mtupu na nawashukuru
kwa zawadi hii ya simu ya kisasa itakayoniwezesha kupiga picha na
matumizi mengine mengi. Alimalizia kusema.
Nae,
Farashuu Hassan mkaazi wa Mbagala alisema “Nilikuwa natumia simu yangu
ndogo isiyokuwa na uwezo wa intaneti lakini sasa nimepata simu yenye
uwezo mkubwa wa 4G ya TECNO R6, itakayoniwezesha kuingia kwenye
Instagram, What’s App na kadhalika ili niwe wa kisasa kwenye ulimwengu
wa mtandao”.
‘Washindi wetu wote 240 tuliowapata kufikia sasa wanatoka sehemu mbali
mbali za nchi, kwa hiyo ninawashauri wateja wetu kote nchini washiriki
ili wajishindie bonasi za data bure pampoja na mojawapo ya simu zaidi ya
800 za Smartphones ambazo bado zinashindaniwa,’ Bushagama alisema.
Kupitia promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo itaongeza idadi ya watumiaji wa simu za kisasa pamoja na matumizi ya data nchini.
No comments :
Post a Comment