Msanii wa muziki Bongo, Diamond
Platnumz anatarajiwa kushiriki katika wimbo maalumu wa Kombe la Dunia
nchini Russia. Wimbo huo utakuwa unawakilisha bara la Afrika.
Wimbo huo umedhaminiwa na
kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola, Diamond atashirikiana na
wasanii wengine kama Sami Dani kutoka Ethiopia, Ykee Benda kutoka Uganda
na Lizha James kutoka Msumbiji.
Hapo awali msanii wa Marekani
Jason Derulo alidokeza juu ya wimbo huo ambao unakwenda kwa jina la
Colors ambao utatoka Machi16 mwaka huu.
Leo Diamond Platnumz kupitia
ukurasa wake wa Instagram ameposti picha inayoashia ushiriki wake katika
Fainali za Kombe la Dunia ambazo zinatarajiwa kufanyika nchini Urusi
kuanzia June mwaka huu.


No comments :
Post a Comment