Kampuni
ya Uchimbaji madini ya Acacia kupitia Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu
(BGML) imekabidhi mradi wa maji kwa wananchi wa kijiji cha Kakola na
mradi wa uzio wa shule kwa shule za msingi Kakola A na B zilizopo katika
kijiji na kata ya Kakola halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani
Shinyanga.
Miradi
hiyo iliyojengwa na wakandarasi wazawa iliyogharimu jumla ya shilingi
milioni 334.9 zilizotolewa na Acacia imekabidhiwa leo Ijumaa Machi
2,2018 na uongozi wa mgodi wa Bulyanhulu kwa Kaimu Mkurugenzi wa
halmashauri ya wilaya ya Msalala,Leonard Mabula.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano hayo,Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa
Bulyanhulu,Jon Almond ujenzi wa miradi hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa
program za kuchangia maendeleo ya jamii ili kuboresha miundombinu ya
jamii na kiuchumi kwenye maeneo yaliyo jirani na migodi.
Alisema mgodi huo umegharamia uwekaji wa uzio “Fence”,yenye
urefu wa kilomita 1.28 kwenye shule hizo mbili kwa shilingi milioni
145.2 kwa kutumia mkandarasi PKM Ltd kutoka mkoa wa Geita.
Aidha
Almond alisema mgodi huo pia umegharamia shilingi milioni 189.6 katika
ujenzi wa mradi wa maji ya kisima kirefu ikiwemo kuunganisha pampu ya
umeme ya kuvuta maji na ujenzi wa mnara wa matanki matano kila moja
likiwa na ujazo wa lita 10,000.
Aliongeza
kuwa ujenzi huo wa mradi wa maji umetekelezwa na wakandarasi kadhaa
wakiwemo HI-GEN Construction Ltd wa Kahama,ENIKON Ltd wa Mwanza na
Namwahi Ltd wa Geita.
“Leo
tuna furaha kubwa kukabidhi miradi hii,mradi wa maji utawanufaisha
zaidi ya wananchi 3000 waliokuwa na changamoto ya maji na uzio huu
utasaidia kuweka mipaka ya shule katika hali ya usalama na wanafunzi
zaidi ya 4000 kuwa katika mazingira tulivu na walimu kufuatilia mienendo
ya wanafunzi wanaotoka na kuingia shuleni”,alieleza Almond.
“Utekelezaji
wa miradi hii umefanikiwa kwa urahisi kutokana na ari ya ushirikiano na
mahusiano mazuri kati ya mgodi ,wananchi na serikali na
kinachofurahisha zaidi ni kwamba miradi hii ilipendekezwa na wananchi
wenyewe kupitia uongozi wa kijiji kama miradi ya kipaumbele”,aliongeza Almond.
Alibainisha
kuwa kumalizika kwa mradi wa maji kunachangia kwenye kipengele cha 10
cha dira ya maendeleo ya Tanzania ifikapo mwaka 2025 inayolenga kuongeza
upatikanaji wa maji safi na salama kwenye maeneo ya vijijini kufikia
asilimia 85 ifikapo mwaka 2020/21 na kwa upande wa uzio wa shule ni
nyongeza ya miradi mbalimbali ya Acacia kusaidia sekta ya elimu.
Akizungumza
wakati wa kupokea miradi hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya
wilaya ya MsalaLa,Leonard Mabula aliushukuru mgodi huo kwa kuendelea
kushirikiana na jamii katika kuwaletea maendeleo na kuwataka wananchi
kutunza miradi hiyo ili iwe endelevu.
“Acacia
wametupunguzia adha ya maji katika eneo hili,naomba wananchi mlinde
mradi huu ili uwe endelevu lakini pia tuutunze uzio huu,uongozi wa
kijiji fanyeni vikao na mikutano mkubaliane namna ya kulinda uzio huu na
mpange bei nzuri ya maji kwa kila mwananchi kuimudu”,aliongeza.
Mabula alisema pamoja na Acacia kuendelea kuisaidia jamii ya Kakola kwa kuwekeza katika miradi ya maendeleo ikiwemo ya maji,huduma za afya,elimu,kilimo,michezo,umeme na miundo mbinu aliomba mgodi kuendelea kusaidia wananchi.
Mabula alisema pamoja na Acacia kuendelea kuisaidia jamii ya Kakola kwa kuwekeza katika miradi ya maendeleo ikiwemo ya maji,huduma za afya,elimu,kilimo,michezo,umeme na miundo mbinu aliomba mgodi kuendelea kusaidia wananchi.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Kaimu
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu, Jon Almond akizungumza wakati wa
kukabidhi mradi wa maji na uzio wa shule kwenye shule za Msingi Kakola A
na B katika kijiji cha Kakola kata ya Kakola halmashauri ya Msalala –
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde1 blog
Kaimu
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Msalala,Leonard Mabula
akizungumza wakati wa kupokea miradi ya Maji na uzio katika shule za
msingi Kakola A na B.
Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Msalala, Leonard Mabula akimpongeza Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu, Jon Almond kwa
kusaidia ujenzi wa miradi mahsusi ya maji na uzio katika kijiji cha
Kakola na kuomba Acacia kuendelea kushirikiana na jamii katika
kutekeleza miradi ya maendeleo.
Katikati
ni Afisa Mawasiliano mgodi wa Bulyanhulu Mary Lupamba akitoa maelekezo
kabla ya zoezi la kukata utepe wakati wa uzinduzi wa uzio ‘fence’ katika
shule za msingi Kakola A na B zilizopo katika kijiji cha Kakola kata ya
Kakola halmashauri ya Msalala.
Kaimu
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Msalala, Leonard Mabula akikata
utepe kuzindua uzio ‘fence’ katika shule za msingi Kakola A na B. Nyuma
yake ni Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu, Jon Almond.
Bango likisomeka “Mradi wa uzio wa shule ya msingi Kakola A na B umefadhiliwa na mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu”. Uzio huo umefunguliwa na Leonard Mabula kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Msalala, Simon Berege.
Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu, Jon Almond akiteta jambo na Kaimu
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Msalala, Leonard Mabula
wakielekea katika mradi wa maji ya kisima kirefu katika kijiji cha
Kakola kwa ajili ya kuufungua.
Eneo la mradi wa maji ya kisima kirefu katika kijiji cha Kakola.
Zoezi la uzinduzi/ufunguzi wa mradi wa maji likiendelea.
Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu, Jon Almond akishikana mkono na Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Msalala, Leonard Mabula wakati wa kufungua mradi wa maji katika kijiji cha Kakola.
Mradi wa Maji Kakola umefadhiliwa na mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu. Mradi huo umefunguliwa na Leonard Mabula kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Msalala, Simon Berege.
Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Msalala, Leonard Mabula na Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu, Jon Almond na wakiwa wameshikilia glasi za maji wakijiandaa kuchota maji na kunywa wakati wa kufungua mradi wa maji.
Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Msalala, Leonard Mabula na Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu, Jon Almond wakinywa maji katika mradi wa maji Kakola wakati wa kufungua mradi huo.
Kaimu
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Msalala, Leonard Mabula
akimtwisha ndoo ya maji Hadija Ponsiano wakati wa kufungua mradi wa maji
Kakola.
Wakazi
wa Kakola wakipata huduma ya maji baada ya mradi kufunguliwa. Kulia ni
Edina Fedrick akipokea pesa kwa mwananchi aliyefika katika mradi huo
kununua maji yanayouzwa kwa gharama nafuu.
Mwanafunzi
wa darasa la saba katika shule ya msingi Kakola A, Nandula Samson
akisoma risala kwa niaba ya wanafunzi wa shule za msingi Kakola A na B.
Alisema wanaishukuru Acacia kwa kuwajengea uzio na sasa watakuwa katika
mazingira salama zaidi.Alieleza kuwa shule hiyo pia inakabiliwa na
upungufu wa vyumba vya madarasa na nyumba za walimu.
Kushoto ni Kaimu Meneja Uhusiano na Ufanisi mgodi wa Bulyanhulu,katikati ni Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu, Jon Almond akifuatiwa na Kaimu
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Msalala, Leonard Mabula
wakisikiliza risala ya wanafunzi wa shule za msingi Kakola A na B.
Afisa
Mtendaji wa kijiji cha Kakola,Daud Simon akizungumza wakati wa hafla
fupi ya makabidhiano ya miradi ya uzio wa shule na maji katika kijiji
cha Kakola.
Mwenyekiti wa kijiji cha Kakola Emmanuel Bombeda akizungumza wakati makabidhiano ya miradi ya uzio wa shule na maji katika kijiji cha Kakola.
Waigizaji kutoka kundi la Nuru kutoka Kakola wakiigiza namna changamoto ya maji inavyotesa jamii.
Wanafunzi wa shule ya msingi Kakola B,waliovaa masweta ya bluu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea.
Wanafunzi
wakiwa wamesimama. Waliovaa masweta ya kijani ni wanafunzi wa shule ya
msingi Kakola A, waliovaa masweta ya bluu ni wanafunzi wa shule ya
msingi Kakola B.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde1 blog
No comments :
Post a Comment